Gasorwe: mufuasi wa chama cha CNL atekwa nyara

Gasorwe: mufuasi wa chama cha CNL atekwa nyara

Viateur Nzigo, mufuasi wa chama cha CNL (kongamano la kitaifa kwa ajili ya uhuru) alitekwa nyara kutoka nyumbani kwake tarafani Gasorwe mkoa wa Muyinga (kaskazini mwa Burundi) asubuhi ya jumatano tarehe 29 machi. Alitekwa na watu waliokuwa ndani ya gari ambalo wakaazi walisema ni gari la idara ya ujasusi. Tangu wakati huo, familia yake haina taarifa zake. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa vyanzo vya SOS Médias Burundi tarafani Gasorwe, gari aina ya Toyota Hilux lilikuja nyumbani kwake. Aliitwa na watu waliokuwa katika gari hilo ambao wajumbe wa familia yake walisema ni askali polisi.

” Polisi hao walimuita wakati bado akilala. Kabla ya kutoka nje, Nzigo alifungua dirisha na kuangalia aliyemuita. Baada ya kugundua kuwa ni askali polisi alitahadharisha wafuasi wenzake wa chama cha CNL. Wanaume hao walimuvamia na kumuweka kwa nguvu ndani ya gari hilo ambalo lilikuwa halina pleti namba “, alifahamisha mjumbe mmoja wa familia yake.

Kulingana na chanzo hicho, polisi hao walimupeleka bila waranti wa kukamatwa, na walikuwa wakielekezwa na mtu aliyekuwa ndani ya gari hilo.

Wafuasi wa chama cha CNL waliotahadharishwa walisema kuwa gali hilo lilitambulika.

” Hakika lilikuwa gari la idara ya ujasusi ambalo lilimupeleka mwenzetu “, alifahamisha mfuasi wa chama cha CNL.

Gari lilielekea kwenye makao makuu ya mkoa wa Muyinga, lakini hadi usiku wa kuamkia jumatano , hakuna aliyekuwa na taarifa kuhusu maeneo anakozuiliwa, au iwapo bado yuko hai.

Familia yake pamoja na wafuasi wa chama cha CNL wanasema kuwa walimutafuta ndani ya magereza yote bila mafanikio. Wanaomba aachiliwe huru.

Previous Goma : a civil society protest to denounce blunders in enrollment centers
Next Bujumbura : waziri wa usalama yazindua warsha iliyoandaliwa na shirika la OLUCOME lakini wajumbe wasimamisha shughuli hiyo