Mahama (Rwanda) : mauwaji ya angalau wakimbizi nane kutoka Burundi yasababisha wasi wasi

Mahama (Rwanda) : mauwaji ya angalau wakimbizi nane kutoka Burundi yasababisha wasi wasi

Uhalifu uliongezeka katika wiki mbili zilizopita ndani ya kambi ya Mahama mashariki mwa Rwanda, inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi na Kongo. Wanaolengwa ni wakimbizi kutoka Burundi huku wale kutoka Kongo wakituhumiwa kutekeleza mauwaji hayo. Wakimbizi wanadai kuwa angalau watu nane waliuwawa na habari kuhusu wawili kati yao zikiwa hamna kabisa. Polisi inaitisha mikutano ya usalama kwa aliji ya kutuliza hali. HABARI SOS Médias Burundi

Kisa cha kushangaza ni wanaume wawili waliokatwa vichwa na watu wasiojulikana karibu ya kambi.

” Hakika ni uhalifu wa hali ya juu. Miili ya watu wawili ilipatikana mwishoni mwa mwezi februari, vichwa vikiwa vilikatwa kwenye umbali wa kilometa mbili nje ya kambi. Badaye walijulikana kama wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambini”, warundi wanaoishi ndani ya kambi ya Mahama walihakikisha.

” Kuhusu mauwaji ya watu wengine wanne, baadhi waliuwawa katika ugomvi , wengine walianguka katika mtego wa vijana kutoka Kongo waliokuwa na fimbo. Ni hali isiokubalika na kwa sasa hali ya taharuki imetanda kambini ikizingatiwa kuwa kuna hata vijana kutoka Burundi waliopotea na ambao hakuna taarifa zao ikihofiwa kuwa waliuwawa tayari “, walizidi kusema viongozi wa jamii ya warundi ndani ya kambi.

Maeneo ya 11, 12, 14, 16,17 na 18 katika upande wa Mahama II yaliathiriwa zaidi na uhalifu huo. Upande huo unapatikana karibu na mto wa Akagera unaotofautisha Rwanda na Tanzania.

Amri ya kutotoka nje ilitangazwa

” Warundi walijipa sharti la kuelekea nyumbani mapema kabla ya usiku kuingia na kutumia pombe wakiwa ndani ya jamii yao. Hatujuwi iwapo ni mpango dhidi yetu lakini tuliahidi kuwa hatutolipiza kisasi. Hata hivyo hatujuwi kuwa hali hiyo itadumu mda mrefu sababu tumevamiwa wazi kabisa na ndugu zetu kutoka Kongo “, wakimbizi kutoka Burundi wanazidi kusema.

Hali ya wasi wasi yazidi kutanda

” Makundi yaanza kujiunda katika maeneo kadhaa ya kambi upande wa wakimbizi wa Burundi pamoja pia na upande wa raia wa Kongo. Harafu ushirikiano kati ya jamii hizo umebadilika ukilinganisha na ilivyokuwa mwezi iliyopita. Hapa habari zinasambaa haraka zilichanganywa na uvumi. Tunahofia hali mbaya zaidi kutokea”, wakimbizi wanazidi kusema.

Kuhamasisha amani

Mikutano ya kuhamasisha amani imekuwa ikiandaliwa na viongozi pamoja na polisi ndani ya kambi.

Ijumaa hii, ilikuwa ni zamu ya kata ya 5 ambako walijumuika wakimbizi kutoka Kongo na Burundi wakaazi wa maeneo ya 11 na 12. Mikutano kama hiyo pia ilifanyika katika maeneo mengine ya Mahama II.

” Viongozi na askali polisi walinzi wa kambi wanatoa ujumbe unaofanana : Ni kuwaomba wakimbizi kuheshimiana, kuwafichuwa watuhumiwa, na kutoa taarifa zote kuhusu hali ya wasi wasi na visa vya uhalifu na kupinga matumizi ya bangi na pombe zilizopigwa marufuku”, wanabaini wakimbizi waliohudhuria mikutano hiyo.

Polisi inawahakikishia na kutangaza kuwa tayari watu zaidi ya kumi walisimamishwa kwa ajili ya uchunguzi juu ya uhalifu huo unaozidi kuongezeka. Wakimbizi wanaomba uchunguzi umalizike na wahalifu waweze kuadhibiwa kwa mjibu wa sheria. Hali hiyo itasaidia kurejesha utulivu ndani ya kambi kama wanavyopendekeza.

Kambi ya Mahama inawapa hifadhi wakimbizi elfu 45 idadi kubwa wakiwa raia wa Burundi pamoja na ma elfu ya raia kutoka Kongo.

Previous Goma-Gavana mwanajeshi kwa wananchi: askali jeshi wa kikosi cha EAC sio maadui zetu
Next Bubanza : kiongozi wa gereza kukamatwa na kupelekwa jela baada ya mfungwa kutoroka