Goma-Gavana mwanajeshi kwa wananchi: askali jeshi wa kikosi cha EAC sio maadui zetu

Goma-Gavana mwanajeshi kwa wananchi: askali jeshi wa kikosi cha EAC sio maadui zetu

Gavana wa kijeshi wa mkoa wa kivu kaskazini aliwaomba wananchi wakaazi wa mkoa huo kuacha kushambulia kwa maneno askali waliotumwa mashariki mwa DRC chini ya kikosi cha kikanda cha jumuiya ya Afrika mashariki (EAC). Wito huo umejumuishwa katika tangazo la ofisi ya luteni jemedali Constant Ndima la jumatano hii.

HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na tangazo hilo, wanajeshi waliotumwa katika mkoa wa kivu kaskazini walikuja kutekeleza makubaliano ya Luanda (Angola) , Nairobi (Kenya) na Addis-Abeba (Ethiopia). Ni makubaliano ambayo serikali ya Kongo ilihusika kwa lengo la kupata suluhu la mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo, alifahamisha luteni kanali Ndjike Kaiko Guillaume msemaji wa serikali ya Kivu kaskazini.

Katika tangazo hilo, serikali ya mkoa inadai kuwa kushambulia kwa maneno vikosi hivyo itawapelekea ” kuanguka katika mtego wa adui”.

” Kwa hiyo, serikali inakariri kuwa ilidhinisha vikosi hivyo vya kikanda kuingia “.

Tangu novemba 2022, kikosi cha kikanda cha EAC tayari kilikuwa kimetuma wanajeshi kutoka Kenya na Burundi mjini Goma. Wanajeshi pia kutoka Uganda na Sudan ya kusini wanasubiriwa.

Hivi karibuni, mandamano mengi dhidi ya kikosi hicho yaliandaliwa katika mji wa Goma ( makao makuu ya Kivu kaskazini) kwa ombi la makundi ya ushawishi na wanasiasa wanaodai kuwa kikosi hicho ” hakiwajibiki na kuegemea upande” kama Monusco ( ujumbe wa umoja wa mataifa nchini DRC) .

Previous Nduta (Tanzania) : kaburi labomorewa na viongozi kwa hoja tu ya kujengwa kwa simenti
Next Mahama (Rwanda) : mauwaji ya angalau wakimbizi nane kutoka Burundi yasababisha wasi wasi