Nduta (Tanzania) : kaburi labomorewa na viongozi kwa hoja tu ya kujengwa kwa simenti

Nduta (Tanzania) : kaburi labomorewa na viongozi kwa hoja tu ya kujengwa kwa simenti

Kitendo hicho kilicholaaniwa na wakimbizi kilitekelezwa kwenye kaburi la mkimbizi wa Burundi, aliyezikwa katika makaburi ya zone ya 9 ndani ya kambi ya Nduta. Ofisi ya mkuu wa kambi ilishuhudia zoezi hilo la kubomoa kaburi la mtu. HABARI SOS Médias Burundi

Katika kambi ya Nduta nchini Tanzania, kuna tukio linaloongelewa sana katika mazungumzo yote eneo la mikusanyiko na maeneo ya umaa. Ni tukio la ” kaburi kubomolewa”kwa ushawishi wa mkuu wa kambi.

” Mama mjaa mzito alikufa tena kwa sababu ya uzembe wa wauguzi. Harafu, familia yake ya kipato cha chini ikamfanyia mazishi na kujenga kaburi lake kwa matofari na simenti. Kaburi hilo likaonekana tofauti katika makaburi hayo ya zone 9″, walibaini majirani wa marehemu.

” Sherehe zingine zinazoambatana na mazishi zilifuata na kuonekana kama sherehe za kutenda msiba wa marehemu katika village 8 ya zone 7″, walizidi kusema.

Wiki tatu badaye, uongozi wa kambi ulitoa amri ya kuvunja kabuli hilo.

” Tulisogelea HCR, mashirika ya kujitolea pamoja na viongozi wa kijamii ili kuomba maelezo zaidi . HCR ilijibu kuwa mkuu wa kambi alitoa amri kuwa makaburi yote yanatakiwa kufanana, hakuna kutumia matofari, semeti ” familia zinafahamisha hayo.

Katika siku ambapo walinzi wa kawaida wanaojulikana kwa jina maarufu ” Sungu Sungu” walikuwa tayari kutekeleza amri hiyo . Familia ilipata taarifa hizo ikapinga mwenendo huo.

” Baada ya mazungumzo marefu na tena ya muda, hatimaye familia binafsi ilibomoa yenyene licha ya kupinga sana.

” Uharibifu wa kaburi na vitisho” …..

Wakimbizi wa Burundi walipinga kitendo hicho.

” Hatuna la kusema. Ni masikitiko, ni kinyume na mila na utamaduni wetu. Huo ni unyanyasaji unaondelea hadi kwenye kabuli la mtu.Ni uharibifu mkubwa wa kaburi”, wakimbizi walieleza hayo na kuhakikisha kuwa walikuwa walipinga taarifa hizo hadi kufika katika makaburi ili kushuhudia kitendo hicho ambacho wanasema kuwa ” ni kitendo cha aibu, cha kikatili na kinyama”. Familia ilipewa amri ya kutotoa taarifa hizo , majirani wa muhanga walihakikisha.

” Kuharibu kaburi, ni kitecho cha kudhalilisha, dhidi ya binadamu na mwisho kitendo hicho kinaathiri kisayikolojia familia ya muhanga”, wakimbizi wa Burundi walisema na kuwaomba viongozi wa Tanzania kulaani kitendo hicho.

Kambi ya Nduta inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi 76 elfu kutoka Burundi.

Previous Burundi: IDHB and Acat-Burundi denounce the continued detention of five Burundian activists
Next Goma-Gavana mwanajeshi kwa wananchi: askali jeshi wa kikosi cha EAC sio maadui zetu