Bubanza : kiongozi wa gereza kukamatwa na kupelekwa jela baada ya mfungwa kutoroka

Bubanza : kiongozi wa gereza kukamatwa na kupelekwa jela baada ya mfungwa kutoroka

Kiongozi wa gereza la Bubanza (magharibi mwa Burundi) Émile Nduwayo alisimamishwa jumatatu baada ya kuripoti mbele ya korti ya rufaa ya Bujumbura ( jiji la kibiashara). Faili hiyo ni baada ya mfungwa mmoja kutoroka. HABARI SOS Médias Burundi

Émile Nduwayezu kiongozi wa gereza la Bubanza alikuwa ametoa ruhsa ya kutoka nje ya gereza kwa habusu mmoja anayejulikana kwa jina maarufu Ngeni alipewa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na faini ya franka za Burundi 555.555 za fidia katika mwaka wa 2013. Aliadhibiwa kwa kosa la mauwaji na wizi.

Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, muhalifu huyo aliomba ruhsa ya kwenda kuchukuwa pesa ndani ya taasisi moja ya fedha eneo hilo tarehe 27 februari iliyopita.

Alikuwa chini ya ulinzi wa askali polisi kwa jina la Evode Hakizimana. Tangu siku hiyo wawili hao hawakurudi kuonekana.

” Walichukuwa njia ya kuelekea Bujumbura badala ya kurudi jela. Walibadili hata nguo ili kijichanganya na raia wa kawaida. Polisi huyo kwa jina la Evode aliyemushindikiza Ngeni hadi sasa hapatikani kwenye simu” vyanzo karibu na faili hiyo vinathibitisha.

Baada ya kufahamu hali hiyo , mkuu wa gereza la Bubanza alitoa taarifa kwa mahakama ya mkoa huo kuhusu utoro huo siku moja baadaye.

Katika siku hiyo pia, aliwasilisha mashtaka dhidi ya Evode Hakizimana.

Uchunguzi uliendeshwa na uongozi wa juu ya idara ya magereza DGAP ndani ya gereza hilo.

Émile Nduwayo alisikilizwa katika mahakama kuu mbele ya korti ya rufaa ya Bujumbura tarehe 6 machi. Alipelekwa badaye katika gereza kuu la Bujumbura maarufu Mpimba kulingana na vyanzo vyetu.

Previous Mahama (Rwanda) : mauwaji ya angalau wakimbizi nane kutoka Burundi yasababisha wasi wasi
Next Mahama (Rwanda) : the assassination of at least eight Burundian refugees creates psychosis