Cibitoke : Zaidi ya waasi wa Rwanda 40 waliuwawa na jeshi la Burundi

Cibitoke : Zaidi ya waasi wa Rwanda 40 waliuwawa na jeshi la Burundi

Takriban waasi 42 wa kundi la watu wa silaha wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda ambao walipiga kambi kwa zaidi ya miaka 10 ndani ya msitu wa Kibira katika tarafa za Bukinanyana na Mabayi mkoa wa Cibitoke (kaskazini Magharibi mwa Burundi) waliuwawa katika mapigano na jeshi la Burundi. Kwa mjibu wa vyanzo, mapigano yalikuwa makali katika wiki tatu zilizopita.
Gavana wa mkoa wa Cibitoke anathibitisha habari hizo lakini amejizuia kuelezea jina la kundi hilo la waasi waliokuwa ndani ya Kibira. HABARI SOS Médias Burundi

Mapigano makali ya wiki tatu zilizopita katika msitu wa Kibira maeneo ya tarafa za Mabayi na Bukinanyana kati ya waasi wa FLN ( Kundi la waasi wenye asili ya Rwanda) na FDNB (Jeshi la burundi) yalisababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali.

” Angalau waasi wa Rwanda 42 waliuwawa na zaidi ya 30 kujeruhiwa vikali na wengine kukamatwa kwenye uwanja wa mapigano. Jeshi la burundi liliwapoteza askali jeshi 11 na wengine kujeruhiwa na sasa wanapata matibabu, lakini maisha yao hayako hatarini”. chanzo cha walinda usalama ambacho hakikutaka jina lake lijulikane kilihakikisha.

Vyanzo vyetu vilizidi na kuonyesha ushahidi kuwa silaha ndogo ndogo zilikamatwa tangu 26 septemba 2022, siku ya kuanzisha rasmi mashambulizi ya jeshi la burundi dhidi ya kundi la FLN.

Wananchi kukimbia

Mapigano hayo yalipelekea wakaazi kukimbilia kwenye vijiji vya Rutorero, Gafumbegeti na Ngara lakini pia kwenye vijiji vya Bumba na Ruhemba, katika tarafa za Mabayi na Bukinanyana.

” Kwa sasa mimi na familia ya watu 11 tuliiacha nyumba yetu na kuelekea kwenye makao makuu ya tarafa ya Mabayi ambapo tulipata hifadhi” , alafahamisha muathiriwa mmoja aliyetiwa woga na mapigano hayo.

Hadi wakati huu, vyanzo vyetu vinakubaliana kuwa hali ya woga na wasi wasi vinawatala wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya mapigano ndani ya Kibira kutokana na mingurumo ya silaha mnamo siku za nyuma.

Hata hivyo kama vyanzo vya utawala vinavyofahamisha, kunashuhudiwa ushirikiano kati ya wananchi na waasi hao kutoka Rwanda ambapo wanabadilishana vyakula na dhahabu inayochimbwa kinyume cha sheria na kundi la FLN katika msitu wa Kibira.

Daima kulingana na chanzo chetu, vijana Imbonerakure ( wajumbe wa tawi la vijana wafuasi wa chama tawala CNDD-FDD) wanahusishwa katika biashara haramu ya dhahabu kwa ushirikiano na waasi hao. Angalau 8 tayari walikamatwa, kwa tuhma za kushirikiana na makundi ya waasi wanaozungumza Kinyarwanda mnamo siku za nyuma.

Waasi hao wanaozungumza Kinyarwanda waliingia wakiwa katika idadi kubwa kutoka Kongo ili kufanya mashambulizi dhidi ya jirani wetu wa kaskazini istoshi kulingana na chanzo chetu cha jeshi mwenye cheo cha juu, kuna baadhi ya askali jeshi wanaowanga mkono.”

Anataja kuwepo na uvunjanji wa habari za kijasusi za kijeshi.
Wakaazi wa kusini Magharibi mwa Rwanda wanasema kuridhishwa na opereshini hiyo dhidi ya waasi wa FLN

Operesheni za kijeshi zinazoendelea zinaungwa mkono na wananchi wa mpakani.

” Tulipigia makofi kazi ilikamilishwa na jeshi la Burundi dhidi ya wahalifu hao wanaosababisha wasi wasi mkubwa miongoni mwa wananchi wa nchi hizi mbili waliotulia ” alibaini mama mmoja wa eneo la Bweyeye katika kanda ya Rusizi kusini magharibi mwa Rwanda.

Gavana wa mkoa wa Cibitoke anathibitisha habari hizo na kuzidi kuwa na operesheni ya kawaida ya jeshi ambayo malengo yake ni kutokomeza makundi yote ya wahalifu ambayo hakupenda kutaja majina. Kuhusu wanajeshi wa Burundi walijeruhiwa na kufariki wakiwa kwenye uwanja wa mapambano, Carême Bizoza anapinga habari hizo na kujizuia kusema chochote juu ya hilo.

Vyanzo vya habari vya kijeshi walihakikishia chumba chetu cha habari kuwa ushirikiano ni mzuri kati ya jeshi la Burundi na Rwanda katika kukabiliana na makundi ambayo ngome zake ziko kwenye msitu wa Kibira yakiwa na uwezo wa kuelekea katika msitu wa Nyungwe ( upande wa Rwanda). Miaka miwili iliyopita, jeshi la Rwanda lilituhumu lile la FDNB kuruhusu waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya Rwanda kuwaruhusu kutumia ardhi ya Burundi na kushambulia nchi ya Rwanda na kurudi, jambo lililopingwa na jeshi la Burundi.

Mikutano ya ma kamanda wa majeshi hayo mawili iliandaliwa kwenye mipaka ya hizo nchi zote mbili za ukanda wa maziwa makuu tangu utawala wa rais Evariste Ndayishimiye kuanza mwezi juni 2020 ili kutafuta jawabu. Burundi upande wake iliituhumu nchi ya Rwanda kuwaacha wapinzani wanaobebelea silaha kufanya mazoezi ya kijeshi kwenye ardhi yake ili kushambulia Rwanda.

Wakuu wa idara za ujasusi za kijeshi walikutana katika mikutano iliyowafikisha kwenye kupeana waasi.

Previous Cibitoke : over 40 Rwandan rebels killed by the Burundian army
Next Burundi: the dry season threatens the country, the government to implores God