Muyinga: Zaidi ya wapinzani 50 wanazuiliwa jela

Muyinga: Zaidi ya wapinzani 50 wanazuiliwa jela

Wananchi ambao kwa sehemu kubwa ni waumini wa dini ya kislam wanazuiliwa katika gereza la polisi Muyinga (Kaskazini-mashariki mwa Burundi) tangu jumapili tarehe 9 oktoba.Wanatuhumiwa kufanya mkutano kinyume cha sheria wa chama cha UPD Zigamibanga tawi la upinzani. Wahusika walikuwa na picha za aliyekuwa kinara wa chama cha CNDD-FDD Hussein Radjabu aliyetoroka nchi tangu miaka saba iliyopita kulingana na vyanzo vyetu. Wako chini ya ulinzi wa polisi. HABARI ya SOS Medias Burundi

Wafungwa hao ni waakazi wa mkoa ya Muyinga, Ngozi na Karusi kaskazini mashariki mwa Burundi. Wanawake idadi yao haijulikani lakini wako katika kiwango cha chini ukilinganisha na wanaume mashahidi wanasema. “Baadhi waliachiwa huru baada ya uchunguzi mfupi. Lakini kwa jumla walikuwa zaidi ya watu 70 alifahamisha askali polisi mmoja kwenye kamishena ya polisi ya Muyinga.Watuhumiwa hao walikamatwa jumapili tarehe 9 oktoba 2022 tarafani Muyinga kata ya Kigwati kwenye makaazi ya mtu kwa jina la Ndiefi, mwalimu kwenye shule ya kipili ya Cumba tarafani Muyinga”, walikuwa katika mkutano majira ya alasiri wakiwa wamekaa kwenye misala inayotumiwa na waislamu wakati wa ibada zao za sala, alithibitisha jirani.

Vijana Imbonerakure kwenye makao makuu ya tarafa ya Muyinga chini ya uongozi wa mkuu wa tawi la vijana hao Shabani walikuja kwa wingi ili kuwakamata. “Wakati walifika, walitulazimisha kulala chini, alifahamisha mmoja aliyechiwa badaye. Wajumbe wa mkutano huo walikuwa wafuasi wa chama cha UPD Zigamibanga tawi la upinzani vyanzo vya habari eneo la tukio vilihakikisha. Walikuwa na picha za Hussein Radjabu, kiongozi wa zamani wa chama cha CNDD-FDD mzaliwa wa tarafa ya Muyinga. Kinara huyo wa zamani wa chama tawala ambaye yuko ukimbizini kwa zaidi ya miaka saba alitoroka gereza kuu ya Bujumbura.”

Ujumbe katika mkutano huo ulikuwa kuwaambia kuwa kuna kundi la waasi linaloundwa na kwamba linatakiwa kuungwa mkono na chama chao”, alibaini polisi mmoja.

Kulingana na vyanzo katika viongozi tawala, baadhi ya wafuasi wa chama cha CNDD-FDD walijichanganya ndani ya kundi hilo wakidai kuwa ni wafuasi wapya.Wanazuiliwa katika gereza la kamishena wa polisi mkoani Muyinga.

Viongozi wa chama cha UPD Zigamibanga, tawi la upinzani hawajasema lolote kuhusiana na madai hayo. Kabla ya uchaguzi wa 2020, wapinzani wengine walikamatwa mkoani Bururi (Kusini mwa nchi). Walituhumiwa kushiriki katika mkutano ambao viongozi tawala waliona ni kinyume cha sheria.Baadhi yao waliachiwa huru hivi karibuni kupitia msamaha wa rais.

Previous Kabarore: walimu walazimishwa kutoa michango
Next Bubanza: Mbunge Fabien Banciryanino aibua mjadala