Rwanda-Burundi: Burundi yatangaza kufungua upya mipaka yake na Rwanda

Rwanda-Burundi: Burundi yatangaza kufungua upya mipaka yake na Rwanda

Ni waziri wa Burundi wa ushirikiano wa kimataifa aliyetangaza hatua siku ya jumanne. Albert Shingiro hata hivyo alikariri nia ya serikali ya Burundi ya kuona Kigali inawafurusha wanamapinduzi inayowahudumia tangu 2015 kwa mjibu wa viongozi tawala nchini Burundi. HABARI SOS Médias Burundi

Waziri Shingiro alitangaza hayo katika jiji kuu la kibiashara Bujumbura kando na mkutano na wandishi wa habari ambapo alitoa ripoti ya yalitokekelezwa na wizara anayoiongoza kati ya julai na septemba iliyopita.

“Tulifungua mipaka yetu na Rwanda lakini hautajaacha sharti letu kuwa wanamapinduzi wanaohifadhiwa na kuwepa chakula na Kigali wanatakiwa kuletwa nchini Burundi […..], tunafikiria kuwa Rwanda, nchi rafiki haitachukuwa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano na nchi yetu na kulipiza kwa kuwahudumia wanamapinduzi hao mjini Kigali ” alifahamisha Bwana Shingiro.

Anawachukulia wanamapinduzi hao kama “wageni wanaleta wasi wasi ” .

” Wanamapinduzi ni wageni wanaleta shida kwa serikali ya Rwanda. Nchi hiyo inatakiwa kutafuta mbinu za kumalizana wao”, alizidi kusema mwanadiplomasia huyo mkuu wa Burundi.

Wanamapinduzi wanaosemekana hapa, walijaribu kuipindua serikali ya hayati rais Pierre Nkurunziza mwezi mei mwaka wa 2015. Muhula wake wa mwisho uliyoleta utata ulifagombaniwa kinyume cha sheria, mahakama ya EAC ilitoa hukumu hiyo.

Mipaka kati ya Burundi na Rwanda imefungwa kwa kipindi cha miaka takriban sita. Hali hiyo ikachochewa na janga la COVID-19.

Kigali upande wake ilifungua mipaka yake na Burundi miezi kadhaa iliyopita.

Previous Rwanda-DRC: the Rwandan government criticizes Congolese authorities for multiplying unacceptable accusations
Next Burundi-UE: Umoja wa ulaya wamusafisha waziri mkuu Gervais Ndirakobuca