Burundi-UE: Umoja wa ulaya wamusafisha waziri mkuu Gervais Ndirakobuca

Burundi-UE: Umoja wa ulaya wamusafisha waziri mkuu Gervais Ndirakobuca

Umoja wa ulaya ulitangaza hatua ya kuondoa vikwazo dhidi ya viongozi wakuu wawili ambao ni waziri mkuu Gervais Ndirakobuca na jemedali Godefroid Bizimana, mmoja kati ya washahuri wa rais Ndayishimiye. Mtu wa tatu ambaye ameondolewa vikwazo na umoja wa ulaya ni aliyekuwa jemedali Léonard Ngendakumana, alikuwa kati ya viongozi wakuu wa idara ya ujasusi ya Burundi na aliyetoroka nchi tangu mwaka wa 2015. Habari hiyo ilijulikana jumanne hii. HABARI SOS Médias Burundi

Baada ya hatua hiyo kutangazwa na ujumbe wa umoja wa ulaya nchini Burundi, wakaazi wa mkoa wa Cibitoke (Kaskazini magharibi mwa Burundi) mkoa wa asili wa viongozi hao wawili walionyesha kuridhishwa na hatua hiyo ya umoja wa ulaya.

Hata hivyo wanaharakati na wajumbe wa mashirika ya kutetea haki za binadamu wanaona kuwa ni kosa kubwa.

” Tumevunjwa moyo na hatua hiyo ya umoja wa ulaya ya kuondoa vikwazo dhidi ya watu walioshiriki katika vitendo vya makosa ya jinai nchini Burundi. Tunafikiri wamekurupuka kuchukuwa hatua hiyo ambayo haijazingatia faida ya muda mrefu na ambayo inaimarisha tabia ya kutoadhibu nchini Burundi. Ni vigumu kuelewa ni misingi gani iliyochukuliwa na umoja wa ulaya ili kufuta vikwazo hivyo sababu mazingatio yaliyosababisha vikwazo hivyo kuchukuliwa hakuna hata moja iliyosuluhishwa. Hatua hiyo ya kuwaondolea vikwazo viongozi wakuu hao wawili kwenye orodha ya umoja wa ulaya inaonyesha kuwa sasa umoja huo haujali tena makosa ya jinai yaliyotendeka nchini Burundi ” anasema Carina Terksakian wa vuguvugu la kutetea haki za binadamu nchini Burundi.

Kwa mjibu wa Anschaire Nikoyagize kiongozi shirika la kutetea haki za binadamu la Iteka, hatua hiyo ni pigo kubwa kwa waathiriwa.

“Hatua hiyo inawaweka pabaya waathiriwa lakini hakuna budi ya kukata tamaa. Ninajaribu kufikiria kuwa sheria itachukuwa mkondo wake licha ya hatua hiyo. Umoja wa ulaya ambaye ni mshirika wa ICC( korti ya kimataifa ya makosa ya jinai) hautaacha haki kwa manfaa ya uhusiano mzuri wa kiplomasia. Ungetakiwa kuendelea kuunga mkono mahakama hiyo ili imalize kazi na hivyo waliofanya makosa waadhibiwe”, anabaini Anschaire Nikoyagize, kiongozi wa shirika la Iteka.

Kwa mjibu wa Christian Ntakirutimana, kiongozi wa shirika la mawakili wanaodai kuwajibika nchini Burundi, ” kama umoja wa ulaya ulichukuwa vikwazo, ni ishara zisizofutika kuwa makosa yalifanyika nchini Burundi. Kwa hiyo umoja wa ulaya utaendelea kuwa shahidi katika mkasa huo siku ambapo haki itatendeka kwa waathiriwa”.

upande wake, Athanase Karayenga mtalaam katika sayansi ya mawasiliano anaona kuwa ” umoja wa ulaya umejidanganya kama unavyofanya kila siku”. Kulingana na yeye, ni uamzi unaowapendelea wale 27 na sio warundi wote kwa jumla.

Baadhi ya mashirika na vyama vya kisiasa wamekaribisha hatua hiyo ” ni hatua ya busara iliyochukuliwa kwa kuzingatia mabadiliko yaliyofanyika nchini Burundi hasa katika sekta ya haki za binadamu”

Furaha pia ni upande wa viongozi wa Burundi. Waziri wa ushirikiano wa kimataifa amechukuwa ukurasa wake wa Twitter kujieleza.
” Ninaridhishwa na hatua ya umoja wa ulaya ya kuwaondolea vikwazo viongozi wa Burundi. Hatua hiyo ni matokeo ya mazungumzo ya kisiasa ya kweli na haki ambayo misingi yake ni nia ya pande zote ya kufufua uhusiano na ushirikiano na Umoja ya ulaya”, ameandika waziri wa Burundi wa ushirikiano wa kimataifa.

kwa mjibu wa mtafiti Terksakian, hatua hiyo inahoji mfumo wa vikwazo vinavyochukuliwa na umoja wa ulaya. Anafafanua kuwa ” serikali zingine zinazokiuka haki za binadamu kwa sasa zitakuwa zikisuburi muda wa kutosha ili umoja wa ulaya uachane na vikwazo na kurudi kwenye ushirikiano kama gisi hakuna kikichofanyika.”

Umoja wa ulaya uliendelea na vikwazo dhidi ya afisa wa SNR ( idara ya ujasusi) Huyo ni Mathias Joseph Niyonzima maarufu kama Kazungu. Anatuhumiwa kutoa mafunzo ya kijeshi kwa Imbonerakure ( vijana wafuasi wa tawi la vijana la chama tawala cha CNDD-FDD) nje ya Burundi na kwenye ardhi ya Burundi. Vijana hao walichukuliwa na umoja wa ulaya kama kundi hasimu na upinzani na walioshiriki katika visa vya kuhujumu wapinzani.

Umoja wa ulaya uliwahi kusema kuwa waliolengwa na vikwazo hivyo walishiriki katika visa vya ukatili na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu.

Previous Rwanda-Burundi: Burundi yatangaza kufungua upya mipaka yake na Rwanda
Next Ryansoro: a dead body spotted