Rwanda-DRC: Uhusiano kati ya hizo nchi mbili za maziwa makuu barani Afrika unazidi kudorora

Rwanda-DRC: Uhusiano kati ya hizo nchi mbili za maziwa makuu barani Afrika unazidi kudorora

Kinshasa iliamuru kumufukuza balozi wa Rwanda siku ya jumamosi. Msemaji wa serikali Patrick Muyaya alifahamisha kupitia tangazo kuwa Vincent Karega amepewa masaa 48 ili awe ameondoka nchini DRC. Rwanda upande wake, imelituhumu kwa mara nyingine jeshi la Kongo kushirikiana na kundi la FDLR linaloundwa na waliofanya mauwaji ya halaiki nchini Rwanda ili kuivuruga kwenye ardhi yake, huku ikichukuwa jamii ya kimataifa kama shahidi. Viongozi wa Rwanda wanasema kusikitihwa na ujumbe wa chuki na kushawishi watu kuvamia raia wa Rwanda na wajumbe wa jamii ya Kongo wanaozungumza Kinyarwanda ambao wanaishi nchi RDC. Wakati huo, kundi la M23, sehemu kubwa wakiwa ni watutsi raia wa Kongo wanaoungwa mkono na Rwanda kwa mjibu wa viongozi wa Kongo linaendelea kudhibiti maeneo mapya. Kundi hilo limechukuwa miji mingine miwili siku ya jumamosi: Rutshuru-makao makuu na kiwanja ndani ya Kivu ya kaskazini. Miji hiyo inapatikana kwenye barabara ya RN2, njia ya kimkakati sababu inaelekea katika mji wa Goma. (Makao makuu ya mkoa wa Kivu ya kaskazini). HABARI YA SOS Medias Burundi

Viongozi wa Kongo wanasema ni muendelezo wa Rwanda wa kuivamia DRC. ” Ilishuhudiwa mnano siku zilizopita ujio kwa wingi wa askali jeshi wa Rwanda kutoa msaada kwa kundi la kigaidi la M23 ili kuweza kushambulia ngome za jeshi la jamuhuri ya Kongo ” alithibitisha bwana Muyaya kwenye televisheni ya taifa.

Rais Tshisekedi ambaye hivi karibuni alituhumu nchi ya Rwanda kuunga mkono kundi la M23 jumamosi aliitisha kikao cha baraza kuu la ulinzi ili kutathimini hali ilivyo mashariki mwa Kongo. Msemaji wa serikali alisema kuwa rais atajieleza mnamo siku zijazo.

” Kutokana na hali ilivyo, baraza kuu la ulinzi limeiomba serikali kumufukuza balozi wa Rwanda nchini DRC Bwana Vincent Karega kwa kipindi kisichozidi masaa 48 tangu kufahamishwa hatua hatua hiyo kutokana na mwenendo wa nchi yake wa kuendelea kuichokoza DRC”. alifahamisha msemaji wa serikali.

Wakati huo, Kiwanja na Rutshuru-makao makuu, miji inayopatikana kwenye umbali wa kilometa 70 kutoka Goma ( makao makuu ya mkoa wa kivu-kaskazini) imeanguka ndani ya mikono ya waasi siku ya jumamosi bila mapigano makali na FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo), kwa mjibu wa mashahidi.

Hata hivyo askali wanne kutoka morroco wa kikosi cha umoja wa mataifa walipigwa risasi, hali iliyopelekea ujumbe huo wa umoja wa mataifa kwa ajili ya usalama (Monusco) kutoa tamko ambamo walikumbusha kuwa mashambulizi dhidi ya askali jeshi wa amani yanachukuliwa kama mauwaji ya kivita. Walizidi kuwa watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha waliohusika na shambulio hilo wamefuatiliwa katika vyombo vya sheria vya ndani na vya kimataifa” aliripoti mwandishi wa radio RFI mjini Kinshasa Patient Ligodi.

Katika siku ya jumamosi, vifaa vya kijeshi na risasi vilivyogunduliwa katika maeneo ya Kiwanja vilikabidhiwa kituo cha wanajeshi wa Monusco na vijana. Takriban wanajeshi 40 wa jeshi la DRC ambao hawakuweza kuondoka kutoka mji huo mapema, walijisalimisha kwenye ngome ya jeshi la umoja wa mataifa, taarifa zinasema.

Rwanda inalaani kufukuzwa kwa balozi wake

Serikali ya Rwanda imepokea kwa masikitiko hatua ya serikali ya Kongo ya kumufukuza balozi wake mjini Kinshasa Vicent Karega, alifahamisha msemaji wa serikali Yolande Makolo.
Katika tangazo la jumapili, Rwanda inafahamisha kuwa wanajeshi wake wako katika tahadhari kwenye mpaka wake na DRC.

” Tunashughulishwa na muungano wa jeshi la Kongo na kundi la FDLR na majaribio yao ya kulenga maeneo ya mipakani na silaha nzito pamoja pia na maneno yao ya chuki dhidi ya Rwanda yanayosambazwa na viongozi wa Kongo” linasisitiza tangazo hilo.
Kwa mjibu wa tamko hilo, Rwanda inaendelea kutahadharisha jamii ya kimataifa juu ujumbe wa chuki dhidi ya raia wa Rwanda unaotolewa na viongozi wa Kongo ambao pia wanashawishi jamii kuvamia raia wenye asili ya Rwanda na dhidi ya jamii ya raia wa Kongo wanaotumia lugha ya Kinyarwanda wanaoishi nchini RDC.

” Kujumuisha kundi la FDLR ndani ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (FARDC) na ushirikiano wao wa moja kwa moja unaendana na hali ya kupanda kwa uvamizi dhidi ya Rwanda na kwa jamii ya raia wa Kongo wanaotumia lugha ya Kinyarwanda ambao wanaishi nchini DRC”, linasema tamko hilo ambalo Yolande Makolo msemaji wa serikali ya Rwanda aliweka kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Nchi ya Rwanda inakariri uamzi wake wa kushiriki katika kutafuta suluhu kupitia majukwa ya kikanda na matokeo ya mikutano ya amani ya kudumu kama yale waliokubaliana Luanda ( Angola) na mchakato wa Nairobi ( Kenya).

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni kwenye radio Rfi na France 24, rais Tshisekedi alisema kuwa “Kundi la FDLR ni kundi ndogo lililogeuka kundi la wezi ambalo haliwezi kuwa tishio kwa Rwanda”.

Hoja zisizokuwa za ukweli

” Ni hoja zisizokuwa na msingi! Ukilinganisha na tuhuma hizo, mimi naona kuwa Rwanda ina nia mbali na inaendelea kutumia sababu hizo ili iweze kuendelea uvamizi wake nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Tangu nilipoanza kuingoza nchi hii yangu, tuliwapeleka mara mbili ma mia ya wapiganaji wa FDLR, huo ni ushahidi wa nia nzuri na kwa sasa ni kundi dogo na haliwezi kuwa tishio kwa usalama wa Rwanda. Haliwezi kutishia usalama wa Rwanda kwa vyovyote vile. ” aliongeza

Kulingana na rais Kongo, “Kundi la FDLR ni tatizo kwetu raia wa Kongo badala ya kuwa tatizo kwa raia wa Rwanda, nikitoa dalili wa mauwaji ya balozi wa Italia nchini DRC Bwana Luca Attanasio aliyeuwawa na kundi la FDLR ambapo sasa limekuwa la kukata barabara, kundi la wezi lisilo na msimamo wa kisiasa wenye lengo wa kuchukuwa utawala wa Kigali kwa hiyo sio hoja za msingi. Ukweli uko mahala pengine ambapo Rwanda inatakiwa kusema.

Kundi la M23 lilichukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021, ni kundi la waasi wa kabila la Batutsi ambalo linaendelea kuchukuwa udhibiti wa maeneo huku likituhumu viongozi wa Kongo ” kuweka mbele njia ya vita kuliko mazungumzo”.

Hadi sasa, kundi hilo linadhibiti maeneo mengi ya mkoa wa Kivu ya kaskazini ikiwemo mji wa Bunagana kwenye mpaka baina ya Uganda.

Mapigano makali yaliibuka tena wiki moja iliyopita kati jeshi la Kongo na waasi na kupelekea ma mia ya wananchi kutoroka makaazi yao.

Baadhi walikimbilia ndani ya miji miwili iliyoanguka katika mikono ya waasi jumamosi, huku wengine wakiwa walielekea nchini Uganda.
Baadhi ya wadadisi wanaona kuwa umoja wa afrika hawujaweka juhudi za kutosha katika kutafuta suhulu la mgogoro mashariki mwa Kongo na kuomba umoja huo kuingilia kati kabla ya kuchelewa .

Previous Cibitoke: farmers complain about the lack of agricultural inputs
Next Giharo: an influential CNDD-FDD member in detention