Bujumbura: uhaba wa mafuta ya gari wajitokeza tena

Bujumbura: uhaba wa mafuta ya gari wajitokeza tena

Waendesha magari wanafanya mlolongo mbele ya vituo vya mafuta katika mji mkuu wa kibiashara wa Burundi ili kupata mafuta tangu wiki mbili zilizopita. Kwenye vituo tofauti, magari yanasimama kwa masaa, mengine kwa ma siku wakisubiri mafuta yafike. Viongozi hawajasema sababu za uhaba huo wa mafuta ambao unavuruga usafiri mjini. HABARI SOS Médias Burundi

Wamiliki wa magari wanalazimika kuyaacha nyumbani. Wengine wananunua mafuka kwenye soko la kienyeji. Wafanyabiashara wa kienyeji wa kuuza mafuta ya gari, wanauzisha lita moja kwa franka elfu 5 wakati ambapo lita moja kwenye kituo cha mafuta ni franka elfu tatu na mia tano.

Katika kipindi hiki cha ukosefu wa mafuta, wafanyakazi kwenye vituo vya mafuta kwa mara kadhaa wanalazimisha wanunuzi kutoa kitita cha ziada hadi elfu 50 kutokana na kiwango cha mafuta wanachotaka kabla ya kupewa.
Jerikani ya lita 25 zinajazwa kwa sharti la kuongeza elfu 30 wakati ambapo wanaendesha pikipiki ambao watataka kujaza matanki yao wanalazimisha kuongeza franka elfu tano ili wahudumiwe.

Athari

Bei ya usafiri kwa texi imekuwa kati ya franka na elfu tatu na elfu 15 badala ya elfu tatu sarafu za burundi bei inayozoweleka. Ni hali inayoathiri ma dereva lakini pia na raia wanaosumbuka kusafiri.
Hali imeanza kuwa ya kutisha, baadhi ya tenki za vituo vya mafuta tayari zimekauka.

Upande wa wizara ya nishati na madini ambayo inafuatilia pia swala la mafuta, hawajathibitisha iwapo ni uhaba.
” Sio swala la uhaba wa mafuta ya gari mjini Bujumbura lakini ni visa vya ukosefu kwenye maeneo tofauti ambako mafuta yamekuwa adimu. Ninawahakikishia kuwa hali inadhibitiwa ” alifahamisha afisa wa juu katika wizara hiyo.

Hata hivyo, uhaba wa mafuta umeshuhudiwa kwa kipindi cha wiki mbili nchini.

Wakaazi wanaanza kupoteza matumaini. Wanahofu kuwa watarudi kwenye ile njia ya msalaba iliyodumu miezi mingi mwaka huu kabla ya kipindi hiki cha wiki kadhaa zilizopita cha upatikana wa kawaida wa mafuta ya gari.

Ukosefu wa sarafu za kigeni ndio chanzo cha uhaba huo kama alivyofahamisha afisa mkuu kwenye benki kuu ambaye jina lake limehifadhiwa.

” Kwa wiki kadhaa mitungi ya kuhifadhi mafuta mjini Bujumbura ni kama mitupu” alihakikisha mfanyabiashara mmoja wa mafuta ya gari.

Rais Neva alithibitisha hivi karibuni kuwa nchi yake haitashuhudia tena uhaba wa mafuta ya gari.

Previous Bujumbura: fuel shortage resurfaces
Next DRC: rais wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo anawatolea mwito raia kukusanyika wote ili kulihami taifa lao dhidi ya "Uvamizi wa Rwanda"