DRC: rais wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo anawatolea mwito raia kukusanyika wote ili kulihami taifa lao dhidi ya “Uvamizi wa Rwanda”

DRC: rais wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo anawatolea mwito raia kukusanyika wote ili kulihami taifa lao dhidi ya “Uvamizi wa Rwanda”

Katika hutba yake kwa taifa, raia wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo alilaani mwenendo wa Rwanda na kuitaja nchi hiyo kama ya kinafki. Anafahamisha kuwa licha ya juhudi za kidiplomasia za serikali ya Kongo, serikali ya Rwanda kwa sababu za ubinafsi, inajihusika na kuvuruga mashariki mwa DRC kwa kuwasaidia kijeshi waasi wa M23. Rwanda ilikanusha daima madai hayo. Na ijumaa hii, rais wa Rwanda Paul Kagame alifahamisha kuwa jeshi la Rwanda halikuundwa ili kuanzisha vita. HABARI SOS Médias Burundi

Rais wa Kongo alisema kuwa ” Mchezo huo wa Rwanda ni kwa ajili ya kujipanulia huku wakitafuta mali za Kongo”

” Ni njama zilizosaidia jeshi la Rwanda kudhibiti eneo la ardhi ya Kongo na kupelekea wananchi zaidi ya laki mbili kutoroka makaazi yao katika wilaya ya Rutshuru pasina msaada” alibaini Bwana Tshisekedi.

Ikizingatiwa hali ilivyo ngumu, Félix Tshisekedi alitoa mwito kwa wananchi kushirikiana kufanya mshikamano wa kitaifa ili kulinda jamuhuri.

Rais wa Kongo aliwaomba pia vijana kuunda makundi kwa ajili ya kupiga doria ili kusaidia na kuunga mkono jeshi la Kongo huku akisisitiza juu ya maelekezo kwa mkuu wa majeshi : Kufungua vituo vya mafunzo ya kijeshi katika mikoa yote ili kuwawezesha wananchi kuingia kwa wingi jeshini kwa ajili ya kulinda na kuhami taifa lao hadi kifo.
” Vita tuliyolazimishwa na majirani yetu inaomba kila mtu kujitolea hadi kukubali kukosa uhai. Ni wakati ya kuachana na tofauti zetu za kisiasa ili kulinda taifa letu mzazi. Mbali na tofauti zetu za kisiasa, itikadi, dini na kabila, kulihami taifa letu ni lengo peke linalotuunganisha kwa wakati huu. Nchi inatutolea wito, taifa linahitaji mchango wa vijana wake na wasichana wake wote “, alithibitisha

Rais Tshisekedi akisisitiza hasa wito wake kwa vijana.

“Kama jibu kwa wito kwa vijana, ninawaalika kujiandaa na kuunda makundi ya kupiga doria [….] Ninarudi kutoa wito kwa vijana wetu ambao wana nia ya kujiunga na jeshi, ninasisitiza juu wito kwa mkuu wa majeshi kuharakisha uanzishwaji wa vituo vya mafunzo ya kijeshi katika mikoa yote 26 ya nchi yetu”, akisisitiza rais wa Kongo.

Mbali na hayo, rais wa jamuhuri alipiga marufuku matamshi yote ya chuki na ubaguzi yanayowalenga watu wa jamii ya wanatumia lugha ya Kinyarwanda ambao wananchi nchini DRC.
” Kisa chochote kinahusiana na hayo, kitaadhibiwa”, alitahadharisha.

Na kuendelea : tunatakiwa kufahamu sisi wote kuwa hakuna mwingine mbadala yetu atakayekuja kulinda taifa letu na inaomba kila mmoja kujihusisha kwa njia zote”.

Aliwaomba pia wanajeshi kuwa wazalendo na kulinda na kuhami nchi na kuhakikisha usalama kwenye ardhi yote ya Kongo na kuepusha uvamizi kutoka sehemu yoyote.

Rais wa jamuhuri alitoa tahadhari wasaliti katika jeshi na wananchi wanaosaidia waasi kuwa wanajiweka katika matatizo ya ugumu wa sheria.

kwa mjibu wa Félix Tshisekedi, kundi la M23 ni lazima liondoke katika maeneo linalodhibiti bila sharti lolote.

Rwanda haijasema chochote kuhusiana na madai ya rais wa Kongo. Lakini rais wa Rwanda Paul Kagame alifahamisha kuwa ” Jeshi la Rwanda halikuundwa ili kuanzisha vita” .
Ilikuwa mbali na sherehe za kula kiapo kwa wanajeshi 500 wapya wa cheo cha juu akiwemo mmoja kati ya watoto wa kiume wa Bw Kagame.

Previous Bujumbura: uhaba wa mafuta ya gari wajitokeza tena
Next Kayogoro: the district administrator sacked