Burundi: vyama vya wafanyakazi vyasikitishwa na kupanda kwa bei ya bidhaa mahitajio muhimu

Burundi: vyama vya wafanyakazi vyasikitishwa na kupanda kwa bei ya bidhaa mahitajio muhimu

Shirikisho la mashirika ya wafanyakazi nchini Burundi Cosybu na CSB wanasema kusikitishwa na hali ya kupanda kwa bei ya bidhaa mahitajio muhimu. Madhara yake ni kupunguka kwa uwezo wa kununua kwa wafanyakazi wa serikali na wananchi kwa jumla. Mashirika hayo yanaomba serikali kuchukuwa hatua za kustaawisha bei. HABARI SOS Médias Burundi

Katika tangazo la chama cha Cosybu na CSB( shirikisho la vyama vya wanunuzi) walieleza masikitiko yao kuhusu kupanda kiholela kwa bei ya mchele, maharagwe, mahindi, mafuta ya gari na vinywaji vya Brarudi (Kiwanda cha kutengeneza vinywaji) .
Mashirika hayo mawili ya wafanyakazi nchini burundi yanafahamisha kuwa kupanda kwa bei ya bidhaa mahitajio muhimu madhara yake ni ” kuporomoka kwa uwezo wa kununua wa wafanyakazi wa umaa”.
Wanaomba serikali kuingilia kati haraka ili kusimamisha changamoto hiyo kwa wafanyakazi wa umaa” kwa kupanda mishahara wakizingatia gharama ya maisha na kuharakisha mchakato wa kupandisha mishahara ya kiwango cha chini kama walivyokubaliana na wadau. Yanaomba serikali pia kupandisha kiwango cha mshahara kinachotakiwa kutolewa ushuru.

kwenye soko, familia za watu wenye kipato kidogo pamoja na wafanyakazi wa serikali wanasema kuwa ” haiwezekani kuishi kwa kutumia mshahara peke”
Kulipa chakula, kodi ya nyumba, kulea watoto, kulipa gharama za matibabu na kumudu mahitaji yote ya familia ni jambo gumu.
Ni vigumu kwa sasa kununua mchele, kilo moja ni kati ya franka za burundi 3150 na elfu 4, wanasema wafanyakazi wa kawaida wa serikali wakati ambapo wali ni chakula ambacho kinakuwa kwenye sahani nyingi za warundi katika miji mingi.
Kilo moja ya maharagwe ya kiwango cha kati ni kati ya 1800 na 2500 kwenye soko la Cotebu mjini Bujumbura (mji mkuu wa kibiashara) .
Rumonge (Kusini-magharibi) hali ya kiuchumi ni ya kusikitisha. Kilo moja ya maharagwe ya kiwango chochote ni kati ya 2200 na 2600 wakati ambapo mwezi uliyopita ilikuwa kati ya 1600 na 2300 sarafu za burundi. Mchele bei yake ni karibu 3500 kilo moja. Kilo moja ya mahindi ni 2000 wakati mwezi uliopita ilikuwa 1600 sarafu za Burundi.

Ili kukabiliana na hali hiyo, vyama vya wafanyakazi vya Cosybu na CSB yanaomba serikali kuchukuwa hatua zinazolenga kupunguza upandaji wa bei hiyo ya bidhaa mahitajio muhimu.

Previous Tanzania: viongozi watawafukuza tena wakimbizi wa zamani wa burundi waliorudi uhamishoni
Next Burundi: boarding schools are no longer able to adequately feed students