Tanzania: viongozi watawafukuza tena wakimbizi wa zamani wa burundi waliorudi uhamishoni

Tanzania: viongozi watawafukuza tena wakimbizi wa zamani wa burundi waliorudi uhamishoni

Kwa jumla, ni raia wa burundi 1048 wanaolengwa na hatua hiyo. Wote ni wakimbizi wa zamani waliorudi ukimbizini katika miaka miwili iliyopita baada ya kurudi nchini Burundi. Walengwa hao wanaomba serikali ya Tanzania kusimamisha hatua hiyo wakidai kuwa “sababu zilizotupelekea kutoroka nchi bado zipo”. HABARI SOS Médias Burundi

Ni kiongozi wa ofisi ya uhamiaji katika kanda ya kigoma ( kaskazini-magharibi mwa Tanzania) aliyefamisha hatua hiyo alhamisi tarehe 3 novemba 2022.
Remegius Pesambili alikuwa amefanya ziara katika kambi ya Nduta nchini Tanzania. Kambi hiyo na ile ya Nduta zinawapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi.
Ma mia ya wakimbizi walikuwa wamealikwa katika mkutano huo ambao uliitishwa kwa lengo hilo.
” Warundi 1048 waliingia ndani ya kambi ya Nduta kinyume cha sheria inayohusu kuomba hifadhi. Tunatoa mfano wa kutokuja kujiripoti kwanza kwenye ofisi ya uhamiaji” alisema.
Kwa mjibu wa Bwana Pesambili, wahudumu wake wanatakiwa kwanza kuchunguza na kuelewa sababu zilizopelekea warundi hao ” kila mara kurudi uhamishoni wakati ambapo nchi yao imerudi kupata amani “.
Hadi wakati huu, walengwa hawapewi msaada wowote, idara ya wizara ya mambo ya ndani inayohusika na wakimbizi haikuwapokea na haiwatambuwi kama wakimbizi.
Wajumbe wa kundi hilo linalokabiliwa na hatari ya kufukuzwa wanafahamisha kuwa ” sababu zilitupelekea kutoroka nchi bado zinashuhudiwa”.
Idadi kubwa ni vijana, watoto na akinamama, alishuhudia mwandishi wa -SOS Medias Burundi.
” Viongozi wa Tanzania wangetakiwa kutusikiliza. Usalama wetu uko hatarini nchini Burundi – ndio sababu tulirudi ukimbizini” walilalamika vijana na akimama hao.
Mwaka wa 2020 viongozi wa Tanzania waliwafukuza warundi wengine 1028. Ilikuwa ni baada ya visa vya mashambulizi ya silaha ndani ya kambi na viunga vyake, visa ambavyo vilidaiwa kufanywa na wakimbizi kutoka Burundi.
Tanzania inawapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi takriban laki moja na elfu 27. Wakimbizi na mashirika ya kutetea haki za binadamu wanatuhumu serikali ya Tanzania kuchukuwa hatua kali dhidi ya wakimbizi kuwalazimisha ” kurudi kwa nguvu” na kulazimisha mashirika ya kiutu kutekeleza hatua hizo kwa lengo hilo.

Previous Tanzania: authorities to expel former Burundian refugees who have returned to exile
Next Burundi: vyama vya wafanyakazi vyasikitishwa na kupanda kwa bei ya bidhaa mahitajio muhimu