Mahama (Rwanda) : mkimbizi wa Burundi afariki dunia baada ya kupigwa na wakimbizi kutoka Kongo

Mahama (Rwanda) : mkimbizi wa Burundi afariki dunia baada ya kupigwa na wakimbizi kutoka Kongo

Emmanuel Ruremesha aliuwawa jumanne hii tarehe 28 februari. Alifariki kutokana na vipigo alivyofanyiwa wakati wa ugomvi na raia wa Kongo usiku wa kuamkia jumanne hii. Polisi tayari ilikamata watu kadhaa kwa sababu za uchunguzi. HABARI SOS Médias Burundi

Ugomvi iliyosababisha kifo cha Ruremesha ulifanyika katika mgahawa wa pombe ndani ya kambi ya Mahama.

” Alipigwa vibaya hadi damu kutililika mdomoni na puwani” mashahidi walieleza.

Licha ya kupelekwa haraka kwenye hospitali ya ” Save the Children” katika zone ya Mahama ll, alifariki dunia siku moja badaye vyanzo vyetu viliendelea kueleza.

Muili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kirehe kwa vile wahudumu wa afya ndani ya kambi wakiwa hawana huduma ya kufanya mazishi.

Baada ya tukio hilo, polisi iliingilia kati na kuwasimamisha watu kadhaa kwa lengo la kufanya uchunguzi.

Watu wa karibu na muhanga, wanaomba muhusika wa mauwaji hayo aweze kuadhibiwa kwa mjibu wa sheria.

Tangu tukio hilo, polisi ilizidisha doria katika eneo la tukio. Wanahofu kuwa warundi wanaweza kulipiza kisasi dhidi ya raia wa Kongo.

Amri ya kufunga mapema mgahawa ilitolewa kwa mmiliki wake.

Amekuwa mkimbizi wa Burundi wa nne kuuwawa katika ukanda huo katika mwezi huu. Wakimbizi wengine wa Burundi waliuwawa katika kambi ya Nduta nchini Tanzania na mwingine katika mji mkuu wa Uganda Kampala mwezi februari ulioyopita.

Previous Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda lauwa mwanajeshi wa tatu wa Kongo
Next Mahama (Rwanda) : a Burundian refugee dies after being beaten up by Congolese