Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda lauwa mwanajeshi wa tatu wa Kongo

Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda lauwa mwanajeshi wa tatu wa Kongo

Jeshi la Rwanda lilifahamisha ijumaa jioni kumuuwa mwanajeshi wa tatu wa Kongo. Kulingana na tangazo, jeshi la Rwanda linafahamisha kuwa mwanajeshi huyo aliyeuwawa alivuka na kuingia katika ardhi ya Rwanda. Ubadilishanaji wa risasi ulifanyika kwenye mpaka kati ya Rwanda na DRC. Hakuna maelezo ya moja kwa moja ya jeshi la Kongo. HABARI SOS Medias Burundi

Tangazo hilo linataka kisa hicho kuwa cha uchochezi. Mwanajeshi wa Kongo aliuwawa alasiri.

” leo (ijumaa) mwanajeshi wa FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kudemokrasia ya Kongo) alivuka mpaka na kufiatua risasi na kuwalenga wanajeshi wa RDF( jeshi la Rwanda) wanaolinda mpaka wa pamoja kati kati ya Petite barrière na Grande barrière katika ukanda wa Rubavu mkoa wa magharibi mwa Rwanda” tangazo hilo lilifahamisha.

Kwa mjubu wa jeshi la Rwanda, wanajeshi wake walijibu risasi hizo na kumuuwa mwanajeshi wa Kongo kwenye ardhi ya Rwanda.

” Wanajeshi wengine wa FARDC walifungua moto dhidi ya jeshi la Rwanda na kusababisha muda mdogo wa kubadilishana risasi”, tangazo hilo linafamisha.

Jeshi la Rwanda lilifahamisha ijumaa jioni kuwa hali ni ya utulivu.

Jeshi hilo lilizidi kusema kuwa kisa hicho ni katika mlolongo wa visa vingine ambapo wanajeshi wa Kongo walivuka mpaka na kuingia kwenye ardhi ya Rwanda.

Hali ni ya wasi wasi

Ijumaa hii jioni, hali ya wasi wasi ilishuhudiwa eno la Birere katika soko dogo eneo la Petite Barrière.

” Raia wa Kongo wengi wakaazi wa Goma ( makao makuu ya Kivu kaskazini) wanataka kuvuka mpaka na kuingia nchini Rwanda wa ajili ya kuanzisha vurugu” alishuhudia mwandishi wa SOS Médias Burundi.

Hukukuwa na maelezo ya moja kwa moja ya viongozi wa Kongo kuhusu mkasa huo. Mwanajeshi wa Kongo aliyeuwawa na jeshi la Rwanda ijumaa hii amekuwa wa tatu kuuwawa na jeshi la Rwanda tangu juni 2022. Katika visa vya awali, viongozi wa Rwanda walikuwa wameeleza kuwa wanajeshi waliouwawa walikuwa wamevuka mpaka na kuanza kupiga risasi kwenye ngome za jeshi la Rwanda, wanajeshi wake wafanyakazi wa idara ya uhamiaji na dhidi ya wananchi.

Tangu kuibuka tena kwa kundi la M23, Kigali na Kinshasa zimekuwa zikituhumiana uchokozi na usaliti. Kundi hilo la waasi la zamani lililochukuwa silaha mwishoni mwa 2021 linatuhumu viongozi wa Kongo kuacha kuteleleza ahadi zake kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kiraia wakiganaji wake. Kwa mjibu wa viongozi wa Kongo, kundi hilo linapata usaidizi kutoka Rwanda.

Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo na kutuhumu viongozi wa Kongo kushirikiana na kundi la waliotekeleza mauwaji ya kimbari nchini Rwanda la FDLR kwa kuwapa silaha risasi na nguo kwa lengo la kusambaratisha ardhi ya Rwanda.

Kwa mara kadhaa, viongozi wa Rwanda walitangaza kuwa ndege za kivita za Kongo zilikiuka masharti ya angani. Jeshi la Rwanda liliwahi kupiga kombora dhidi ya ndege ya kivita ya Kongo.

Hivi karibuni, jeshi la Rwanda lilifahamisha kuwa limerudisha nyuma uvamizi wa wanajeshi wa Kongo kati ya 12 na 14 kati ya mkoa wa Kivu kusini na kanda ya Rusizi magharibi mwa Rwanda daima.

Jeshi la Kongo lilipinga madai hayo na kusema kuwa badala yake lilikuwa kundi la watu wa silaha ambalo lilishambulia ngome yao karibu na mpaka na Rwanda, na kutuhumu Rwanda ” kupata hoja ya kuvamia mkoa wa Kivu kusini kama ilivyofanya ndani ya Kivu kaskazini “.

Jumatano hii katika mkutano wake na wandishi wa habari, rais wa Rwanda Paul Kagame alikumbusha kuwa ” tuko tayari kijihami tangu muda mrefu”, na kuhakikisha kuwa wahusika wa usalama wa Rwanda walijiandaa tangu zamani”. Alikuwa akijieleza kuhusu uhusiano mbaya kati ya nchi yake na DRC.

Viongozi wa ukanda huu wanasumbuka kupata suluhu la mzozo wa usalama unaoripotiwa mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati na mjumbe wa jumuiya ya afrika mashariki.

Previous Mahama (Rwanda) : Bidhaa za vyakula zimepanda bei kwa kiwango kikubwa
Next Mahama (Rwanda) : mkimbizi wa Burundi afariki dunia baada ya kupigwa na wakimbizi kutoka Kongo