Mahama (Rwanda) : Bidhaa za vyakula zimepanda bei kwa kiwango kikubwa

Mahama (Rwanda) : Bidhaa za vyakula zimepanda bei kwa kiwango kikubwa

Kwa kipindi cha angalau miezi mitano, takriban bidhaa zote mahitajio muhimu zilipanda bei mara dufu na hata mara tatu. Wakimbizi wanadai kuwa pesa wanazopewa hazitoshi kukidhi mahitaji yao hata kwa wiki mbili wakati ambapo pesa hiyo inatakiwa kutumiwa kwa kipindi cha mwezi bila kutaja ucheleweshaji wa pesa hiyo. HABARI SOS Médias Burundi

Vyanzo vyetu vilifanya makadirio ya bei ya vyakula muhimu kwa kipindi cha miezi mitano. Wakimbizi hawawezi kumudu bei.

” Kilo cha maharagwe kilichokuwa kati ya franka 650 na 800 sarafu za Rwanda kilipanda hadi 1100 na 1300 sawa na viwango cha maharagwe hayo , kilo moja ya ndizi sasa ni 400 wakati bei ilikuwa 200 huku viazi ulaya bei ya kilo moja ilitoka kwenye franka za Rwanda 350 hadi 700. Bidhaa zingine kama viazi utamu, mihogo na mboga boga ambazo haziuzishwi kwa kupima uzito badala yake kwa mifungo zilipanda mara dufu na mara tatu, kadhalika mchele , unga wa mahindi na mafuta ya kupikia. Hata maziwa yalipata bei kutoka 250 hadi 350 sarafu za Rwanda nusu lita”, alifafanua mkimbizi kutoka Burundi.

Baya zaidi kulingana na wakimbizi, ” hakuna anayeweza kununua nguo au viatu, watoto wanatembea miguu wazi na wengine kifua wazi”.

Msaada hautoshi…….

Mwanzoni mwa mwezi februari iliyopita, kiwango cha mgao wa chakula kiliongezwa kwa baadhi ya wakimbizi. Kitita cha pesa wanachopewa kila mwezi na kwa kila mkimbizi wa Mahama kilikuwa 7000 sarafu za Rwanda na (7 USD) na kufikia 10.000 Frw ( 10 USD ) kwa wakimbizi mafukara ( kiwango cha l) na 3.500 Frw hadi 5.000 Frw kwa wakimbizi wengine (kiwango cha kijamii ll).

WFP inaeleza kuwa hatua hiyo ni kwa lengo la kuboresha maisha ya wakimbizi wakati huu ambapo maisha yamekuwa ghali.

” Ikizingatiwa kupanda kwa bei katika soko ndani ya Kambi ya Mahama na viunga vyake, PAM ilizungumza na HCR pamoja na Minema, wizara inayohusika na wakimbizi. Matokeo ya mazungumzo hayo ni kuongeza kiwango cha pesa inayopewa wakimbizi kila mwezi ” shirika la WFP (PAM) lilifahamisha.

Licha ya kupokelewa vizuri, hatua ya kupandisha kiwango cha pesa hiyo bado hakijatosha kulingana na wakimbizi.

” Ukiangalia matumizi ya nyumbani, pesa hiyo haiwezi kutosha hata kwa kipindi cha wiki mbili wakati ambapo inatakiwa kutumiwa siku 30 . Na kama ni familia ndogo, au familia ya mtu mmoja, chakula hakipatikani kwa sehemu kubwa ya mwezi na hivyo inakuwa vigumu sababu familia ndogo hupata kiwango kidogo cha msaada”, wakimbizi wanalalamika.

Maoni yanatofautiana, baadhi ya wakimbizi wanapendekeza PAM irudi kwenye mfumo wa zamani wa kugawa chakula na hivyo waweze kuwa na matumaini ya kupata chakula mwezi mzima. Wengine wanapendekeza mashirika ya misaada yaongeze kiwango cha misaada inayotolewa ndani ya kambi hiyo inayozidi kukuwa kutokana na ujio wa wakimbizi kutoka Kongo mnano siku zilizopita.

Kambi ya Mahama inayopatika mashariki mwa Rwanda huorodhesha zaidi ya wakimbizi 45 elfu idadi kubwa ikiwa ni wakimbizi kutoka Burundi, wanaosalia wakiwa wakimbizi kutoka Kongo.

Previous Ituri: zaidi ya wananchi 200 waliuwawa na waasi katika kipindi cha miezi miwili
Next Rwanda-DRC : jeshi la Rwanda lauwa mwanajeshi wa tatu wa Kongo

About author

You might also like

Health

Nyarugusu : yafungwa maduka ya dawa yasiyojulikana

Uwindaji wa wamiliki wa maduka ya dawa yasiyokuwa halali ulianzishwa ndani ya Nyarugusu. Shirika la Medical Team International linalohusika na sekta ya afya lina mpango wa kukataza tabia ya kujitibu

Economy

Burundi : inhabitants of Bujumbura city can no longer bear the high cost of living

The population of the commercial city Bujumbura is indignant at the excessively high prices of foodstuffs on the market. Families are no longer able to provide three meals a day

Refugees

Rwanda : HCR yatafuta wakimbizi kwa ajili ya Canada

HCR-Rwanda iko kwenye hatua ya kuhamasisha jamii ya wakimbizi kwa ajili ya kuhamia nchini Canada kwa sababu za kiuchumi. Baada ya Kigali, ni zamu ya kambi ya Mahama. Lengo :