Ituri: zaidi ya wananchi 200 waliuwawa na waasi katika kipindi cha miezi miwili

Ituri: zaidi ya wananchi 200 waliuwawa na waasi katika kipindi cha miezi miwili

Tangu mwanzo wa mwaka 2023, hali ya usalama inazidi kuwa ya wasi wasi na kusikitisha katika mkoa wa Ituri karibu miaka miwili tangu kuanzisha serikali ya kijeshi. Wananchi wa kawaida wanaendelea kuuwawa na makundi ya silaha ya ndani na nje katika wilaya nyingi za mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC. Mashirika ya kiraia yanatoa orodha ya wananchi wa kawaida 226 waliouwawa na makundi ya silaha katika miezi ya januari na februari. HABARI SOS Médias Burundi

Takwimu hizo ni za muda kulingana viongozi wa mashirika ya kiraia eneo hilo.

” Kuhusu hali ya februari 2023, tulihesabu watu 78 waliouwawa, 10 walijeruhiwa, 28 walitekwa, pikipiki 4 ziliibiwa na nyumba 379 kuchomwa moto. Hasabu hizo zinaongeza idadi ya waliouwawa kufikia watu 226 tangu januari 2023 hadi 28 februari 2023. Takwimu hizo zinasalia kuwa za muda”, anasema Dieudonné Lossa muakilishi wa shirika la wazalendo la Ituri.

Pamoja na hayo, analaani kuwa wakimbizi wa ndani wanaishi katika hali ngumu bila msaada wa serikali wala wa mashirika ya ndani na kimataifa.

Kwa kizingatiwa hali hiyo mbaya ya usalama eneo la Ituri, mashirika ya kiraia yanaomba serikali ya Kongo kuongeza idadi ya wanajeshi katika eneo lote la mkoa huo kwa ajili ya kulinda wananchi na mali zao.

Makundi mengi ya nje na ndani likiwemo kundi la ADF ( Nguvu zilizoungana kwa ajili ya demokrasia) yamekuwa chanzo cha mauwaji ya wananchi katika wilaya ya Irumu na Mambasa.

Mkoa wa Ituri pamoja na mkoa jirani wa Kivu kaskazini iko katika hali ya taharuki na utawala wa kijeshi tangu mei 2021, mfumo ambao hawukuweza kumaliza tatizo la usalama mdogo linaloendelea katika eneo hilo la Kongo.

Previous Rwanda-DRC : Rwandan forces killed a third Congolese soldier
Next Mahama (Rwanda) : Bidhaa za vyakula zimepanda bei kwa kiwango kikubwa