Minembwe: mwanajeshi amuuwa mwanafunzi kwa panga

Minembwe: mwanajeshi amuuwa mwanafunzi kwa panga

Mugaza Nganganyi (Miaka 16) aliuwawa jumapili hii. Ni mwanajeshi wa FARDC (Jeshi la jamuhuri ya Kongo) aliyemuuwa kulingana na familia yake. Alimufananisha na raia wa Rwanda. Muhanga ni mjumbe wa jamii ya Banyamulenge. Muuwaji alikamatwa. HABARI ya SOS Medias Burundi

Ni eneo la Minembwe katika kanda ya Fizi, mkoa wa kivu-kusini mashariki mwa DRC ambako kisa hicho kilifanyika. Ilikuwa siku ya jumapili 9 oktoba 2022.

Kwa mjibu wa mashahidi, mwanajeshi huyo alitumia panga ili kumuuwawa kijana huyo wa kiume.

” Mwanajeshi huyo alikuta mtoto wetu eneo la karibu ya kambi ya kijeshi la FARDC ambako anachunga ng’ombe. Alimuuwa kwa mapanga ” walifahamisha wajumbe wa familia yake kwa SOSMedias Burundi.
Na kuzidi kuwa ” baada ya kisa hicho cha ukatili, mwanajeshi huyo alikata mkono mtoto wetu. Aliupeleka kambini kuonyesha wenzake kuwa ameuwa adui kutoka Rwanda.”

Vyanzo vya kijeshi katika mkoa wa Kivu ya kusini walihakikishia chumba chetu cha habari kuwa aliyefanya mauwaji hayo alisimamishwa. Anazuiliwa ndani ya gereza la jeshi.

Siku ya jumamosi, wanajeshi wengine chini ya uongozi wa André Ekembe waliuwa ng’ombe watatu katika kijiji cha Kalingi daima mkoa wa Kivu ya kusini kulingana na vyanzo eneo hilo.

Jumatatu hii, walimu na wanafunzi wa eneo la Minembwe waliteremka barabarani katika mandamano ya amani ili kushinikiza haki dhidi ya kijana Mugaza itendeke.Wakuu wa jeshi na viongozi wa raia hawajatoa tamko lolote baada ya janga hilo.

Previous Rutana: resurgence of domestic violence and murders of spouses in the provincial capital
Next Minembwe : kundi la Mai Mai limemuuwa mzee mmoja na kupora ng'ombe 150