Minembwe : kundi la Mai Mai limemuuwa mzee mmoja na kupora ng’ombe 150

Minembwe : kundi la Mai Mai limemuuwa mzee mmoja na kupora ng’ombe 150

Ndagara Buhimba (Miaka 80) aliuwawa siku ya jumatatu alasiri. Kundi la Mai Mai lilirejuhi pia watu 2 na kuiba ng’ombe 150. HABARI ya SOSMedias Burundi

Muhanga alikuwa katika malisho yaliyo katika eneo la Monyi wakati waasi wa Mai Mai waliopomuuwa kulinga na mashahidi.Ni katika kanda ya Minembwe wilaya ya Fizi katika mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC.

Kifo cha mzee huyo kutoka jamii ya Banyamulenge kinathibitishwa na familia yake.

” Asubuhi hii ndipo muili wake umepatikana.Ni vitendo vya kinyama vinavyofanyika hapa. Watu wanauwawa kama wanyama wanachinjwa”, amelalamika mkaazi mmoja.

Vyanzo sehemu hiyo vinahakikisha kuwa watu wengine wawili walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo ‘a ng’ombe 150 kuibiwa.

Msemaji wa kundi la Mai Mai hakuwa karibu ili aweze kujieleza juu ya malalamiko hayo. Wakuu wa jeshi na viongozi tawala pia hawajasema lolote.

Siku ya jumapili, kijana mdogo aliuwawa kwa kukatwa na panga na askali wa jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ) katika eneo hilo la Minembwe , kisa ambacho kilisababisha mandamano katika shule zote ijumatatu eneo la Minembwe.

Wakaazi wa eneo la Minembwe ambao wengi wao ni kutoka jamii ya Banyamulenge wanalituhumu jeshi la Kongo kutuwahami wakati wakilengwa na mashambulizi ya makundi ya silaha.

Ni tangu miaka mitano tukiuwawa bila hata hivo jeshi la FARDC kuingilia kati ili kutulinda wakati ambapo tuko raia wa Kongo ” analalamika diwani mmoja

Previous Minembwe: mwanajeshi amuuwa mwanafunzi kwa panga
Next Burundi : Vijana ambao hawajafunga ndoa hawana ruhsa ya kutumia mipango ya uzazi wa majira (waziri wa afya)