Burundi : Vijana ambao hawajafunga ndoa hawana ruhsa ya kutumia mipango ya uzazi wa majira (waziri wa afya)

Burundi : Vijana ambao hawajafunga ndoa hawana ruhsa ya kutumia mipango ya uzazi wa majira (waziri wa afya)

Waziri wa afya Sylvie Nzeyimana alifahamisha hayo siku ya jumanne katika mji mkuu wa biashara Bujumbura. Ni kando ya kongamano kuu la akinamama viongozi.
Kwa mjibu wa waziri Nzeyimana, waliofunga ndoa peke ndio wanaohusishwa na mipango wa uzazi wa majira. HABARI ya SOS Medias Burundi

Akijibu swali wakati wa muelezo wake kando na mkutano mkuu wa akinamama viongozi, Daktari Sylvie Nzeyimana amesema hayo kwa dhahiri.

” Vijana wanatakiwa kufundishwa kuhusu afya ya uzazi. Hawawezi kufanya tendo la ndoa kwa sababu linafanywa na watu waliofunga ndoa peke” alibaini hayo waziri Nzeyimana kando na kongamano kuu la akinamama viongozi ijumanne hii.

Hata hivo amemuomba waziri wa elimu kuongeza mikutano ya kuhamasisha kuhusu uzazi wa majira mashuleni.

Kwa mjibu wa takwimu za serikali ya Burundi, asilimia 38 ya akinamama walijiunga na mpango wa uzazi wa majira katika nchi hii ndogo ya afrika mashariki.

Mashirika ya vijana wao wanafahamisha kuwa vijana kati ya miaka 15 na 24 wako katika hatari ya kufanya ngono bila kijilinda.

” Serikali na mashirika ya vijana wanakatiwa kukaa pamoja na kujadili njia nzuri ambayo kundi hilo wanaweza kunufaika na uzazi wa majira sababu ni kundi ambalo liko katika hatari kubwa”, ni mtazamo wake mwandishi wa habari wa Burundi anayefuatilia kwa karibu habari kuhusu mpango wa uzazi wa majira .

Kwa mjibu wa katibu wa shirika la akinamama kwa ajili ya amani na usalama, vijana wa kike wanatakiwa kufikiwa na huduma ya uzazi wa majira kwa sababu ” wako katika hatari ya kufanya ngono bila kujikinga na kubakwa kutokana na sababu nyingi zikiwemo zile za umasikini”.

Anaomba wazazi kuendelea na jukumu lao kwa kuzungumza na watoto wao kuhusu swala la ngono na mila na desturi za warundi, jambo ambalo anawaomba pia waziri.

Previous Minembwe : kundi la Mai Mai limemuuwa mzee mmoja na kupora ng'ombe 150
Next Bubanza: five thousand households expropriated ask to be relocated