Ituri: watu takriban 30 wameuwawa eneo la Djugu

Ituri: watu takriban 30 wameuwawa eneo la Djugu

Shumbulio jingine la mauwaji lilifanywa na kundi la CODECO ( shirikisho kwa ajili ya maendeleo ya Kongo) katika wilaya ya Djugu Kijiji cha Bahema-Banywagi kwenye kitongoji cha Nyamamba wekendi hii. Mashirika ya ndani yanafahamisha kuwa waasi walifanya shambulio hilo kwenye mwambao wa ziwa Albert ambako waliwauwa watu 31, 24 kati ya hao waliuwawa katika kitongoji cha Nyamamba huku saba wengine wakiuwawa katika kitongoji cha Mbongi eneo la Lossandrema ndani ya Kijiji cha kaskazini-Bahema. HABARI SOS Médias Burundi

Mashirika ya kiraia ya ndani yanafahamisha kuwa watu wengine hawajulikani walipo tangu shambulio hilo kutokea siku ya jumamosi iliyopita.

Watetezi wa haki za binadamu wanalaani kuona hadi sasa jeshi bado halijaingilia kati.

SOSMedias Burundi ilijaribu kuwasiliana na msemaji wa operesheni za kijeshi wilayani Ituri bila mafanikio.

Kanda hiyo inakabiliwa na tishio la mashambulizi ya makundi ya silaha ya ndani na nje likiwemo kundi la CODECO ( Nguvu zilizoungana kwa ajili kidemokrasia). Tangu tarehe 8 januari 2023, angalau raia wa kawaida 66 waliuwawa katika wilaya ya Djugu na Irumu na Ituri kulingana na takwimu zetu.

Waliuwawa katika mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na makundi mawili ya silaha licha ya hatua za kusitisha mapigano kufikiwa mwezi disemba mjini Nairobi (kenya) wakati wa awamu ya tatu ya mazungumzo kuhusu mzozo wa Kongo.

Previous Musigati: wakaazi wahofia njaa
Next Bijombo: Twirwaneho fighters killed three FARDC soldiers