Musigati: wakaazi wahofia njaa

Musigati: wakaazi wahofia njaa

Hofu ya uwezekano wa kutokea baa la njaa inazidi kuwakumba wakaazi wa tarafa ya Musigati. Bei ya bidhaa mahitajio muhimu imeongezeka mara dufu na hata mara tatu. Wafanyabiashara wanasema ni kutokana na uhaba wa mavuno ya ndani. HABARI SOSMedias Burundi

Mvua zilichelewa kunyesha, na mavuno yakawa mabaya.

” Nyakati kama hizi, maharagwe na mahindi mabichi huwa yanakuwa mengi lakini kwa sasa hamna kwenye masoko”, aligundua mununuzi mmoja aliyekuwa akitafuta maharagwe kwenye soko tarafani Musigati.

Bei ya baadhi ya bidhaa ilipanda mara tatu, kilo moja ya maharagwe hununuliwa franka za burundi 3500.

” Ni mara ya kwanza kwa bei ya maharagwe kupanga kwa kiwango hicho”, alalamika mfanyakazi mmoja wa serikali anayekiri kuwa anapata usumbufu kupata chakula cha mwezi kwa familia yake.

Bidhaa za vyakula zingine ambazo zilikuwa zikizalishwa kwa wengi tarafani Musigati sasa ni adimu na bei ni kubwa. Mfano ni ndizi. Bei ya ndizi mmoja ni franka elfu 15.

Migomba ya ndizi ilipigwa na aina ya wadudu kulingana na mafundi wa kilimo.

Sera ya kilimo cha mpunga katika mabonde kwa udhamini ya miradi inayofadhiliwa na FIDA ( fuko la kimataifa kwa ajili ya kuendeleza kilimo), hadi katika maeneo ambako kilimo hicho hakijawahi kufanyika, haikudhibiti mfumoko wa bei ya mchele. Bei ya kilo moja ya mchele ni franka 3600 kwenye soko la Bubanza. Tarafani Musigati ni franka 4000.

” Tutakabiliwa na maradhi ya utapia mlo “, analaumu mkaazi wa eneo la Kivyuka katika tarafa hiyo mwenye umri wa miaka takriban 60. Kwa familia ya wastani ya watoto 6 mkoani Bubanza, pesa inayohitajika kwa mlo mmoja ni franka za Burundi 5000

Hayo ni wakati kwa siku mmoja mfanyakazi za mikono hupokea kati ya 2500 na 3000 mkoani Bubanza.

” Tuna watoto ambao watapewa vidongi kwenye hospitali tarafani Musigati, ni aina ya vidongi kwa ajili ya wale wanakabiliwa na utapia mlo. Ni lazima vidongi hivyo viongezwe anaomba mwanamke mmoja ambaye alikutwa eneo la Kivyuka.

Anapambana katika biashara ya viazi ulaya anavyonunua kwa wafanyabiashara wanaolangua mkoani Kayanza ( kaskazini mwa Burundi).

Mteule mmoja katika tarafa hiyo alizungumzia swala hilo.

” Hakuna mavuno katika msimu huu wa A. Hayo ni kutokana na mvua kuchelewa kunyesha, pamoja na ukosefu wa mbolea ya kizungu”.

Na kuzidi ” ardhi yenye milima na mabonde ya Bubanza haina uzalishaji tena wa kutosha”.

” Tuna wateule katika chama cha CNDD-FDD katika tarafa yetu, kwa hiyo serikali ingetakiwa kufanya kila kitu kwa kuacha ushuru wa bidhaa za vyakula kwa mfano. Hivyo, Wafanyabiashara hawatakuwa tena n’a hoja za kuuzisha kwa bei kubwa” anapendekeza mteule mmoja.

Kulingana na ofisi ya mazingira, kilimo na ufugaji mkoani Bubanza, mfumoko wa bei ya bidhaa za vyakula ulisababishwa na kuchelewa kwa mvua kunyesha. Afisa wa kilimo katika mkoa huo ana matumaini kuwa mavuno yatakuwa mazuri katika msimu wa kilimo wa B.

” Kupunguka kwa bei kutasababishwa na upatikanaji wa mavuno ya kutosha lakini pia ni muhimu watu kufahamu kuwa idadi ya watu iliongezeka sana”, amefafanua kiongozi huyo.

Previous Gahuna: jeshi la FARDC na FDND wamesimamisha watu watano wakiwemo warundi wawili
Next Ituri: watu takriban 30 wameuwawa eneo la Djugu