Gahuna: jeshi la FARDC na FDND wamesimamisha watu watano wakiwemo warundi wawili

Gahuna: jeshi la FARDC na FDND wamesimamisha watu watano wakiwemo warundi wawili

Watu hao watano raia wa kawaida walisimamishwa jumamosi hii majira ya alasiri : wanatuhumiwa kumuhudumia kanali Makanika, kamanda wa kundi la Twirwaneho linaloundwa na watu wa jamii ya Banyamulenge. HABARI SOS Médias Burundi

Watu hao walikuwa wakielekea katika eneo la Nyawaranga. Ni katika kijiji cha Bijombo, wilaya ya Uvira ( mkoa wa kivu ya kusini mashariki mwa DRC), kwa mjibu wa vyanzo vya ndani.

Visa hivyo vilitokea katika kijiji cha Kibogero.

” Ni wachungaji wawili, raia wa Kongo kutoka jamii ya Bashi, mkuu wa kijiji cha Gahuna pamoja na kijana ambaye ni kati ya walinzi wa karibu wa kanali Makanika” , vyanzo vya kijeshi vinasema.

Kulingana na vyanzo eneo la Bijombo, wapiganaji wa Twigwaneho walitoa amri kwa watu hao waliokuwa wanazuiliwa ” kubeba vyakula hadi eneo la Nyawaranga”.

Taarifa kutoka katika vyanzo vya jeshi zinahakikisha kuwa wahusika wanazuiliwa katika mji wa Uvira.

Kulingana na wandishi wetu, katika eneo hilo la Kongo ambako makundi ya silaha ya ndani na nje kutoka Burundi yalipiga kambi, makundi ya waasi yanatumia raia wa kawaida kubeba vyakula na risasi, eneo hilo likiwa halina barabara.

FDNB ( jeshi la Burundi) liko katika ardhi ya Kongo rasmi tangu agosti 2022. Wanapatika eneo hilo chini ya mwamvuli wa kikosi cha kikanda cha EAC kilichoanzishwa na wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki juni mwaka jana. Lakini jeshi la Burundi kwa miaka mingi linatuhumiwa kuingia kwenye ardhi ya Kongo wakiwa pamoja na vijana wafuasi wa tawi la vijana la chama tawala cha CNDD-FDD kulenga hususan kundi la FNL( waasi wa Burundi) na Red-Tabara, kundi linalochukuliwa na viongozi wa Burundi kama kundi la kigaidi, makundi hayo mawili yakiwa yalipiga kambi eneo la Kivu kusini.

Katika miezi iliyopita, mapigano kati ya jeshi la Burundi na makundi hayo mawili ya silaha yaliripotiwa eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini na kila upande ukidai kupata ushindi.

Previous Musigati: residents fear famine
Next Musigati: wakaazi wahofia njaa