Bubanza: idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na njaa yaongezeka

Bubanza: idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na njaa yaongezeka

Wakaazi ya kijiji cha Buhoro tarafa na mkoa wa Bubanza (magharibi mwa Burundi) wanasikitishwa na kupanda kwa bei ya nafaka za vyakula. Kwenda shule bila kutia kitu tumboni ni jambo lisilowezekana kwa idadi kubwa ya wanafunzi. Waliamuru kuacha shule. Kiongozi mmoja wa shule alifahamisha kuwa ni takriban 20 walioacha shule katika eneo lake peke. Familia nyingi zinasema kuwa “hatuna uwezo wa kupata chakula cha kutosha watoto wetu”. HABARI SOS Médias Burundi

Mwishoni mwa mwezi wa septemba, bei ya nafaka za chakula ilipanda katika hali ya kusikitisha mkoani Bubanza na katika mikoa mingine ya nchi hiyo ndogo ya afrika ya kati.

Mchele, mahindi, unga wa mihogo na vingine…vilipanda kwa franka elfu moja kilo moja hata na zaidi. Hivyo ndio chakula cha kawaida kwa warundi kwa jumla.
Vyakula ambavyo bei haikupanda ni pamoja na mihogo, viazi na mahole.
” Familia wanapata kwa tabu mlo mmoja kwa siku, chakula cha usiku”, anahakikisha mama moja.

Mwendesha pikipiki anasema kuwa anapata usumbufu wa kulisha familia yake.

” Inatokea kuwa ninapata elfu 3 sarafu za burundi kwa siku wakati hiyo ni bei ya kilo moja ya mchele. Bei ya maharagwe ni 2300 sarafu za burundi kwa kilo moja, unga wa mihogo 1700 harafu unga wa mahindi bei yake ikiwa 2300 kilo moja. Siwezi kutosheleza familia yangu na pesa hiyo ninayopata” , analalamika.

Athari za uhaba huo wa nafaka za vyakula

” Niliona watoto wenye muonekano kama wa watoto wanaokabiliwa na utapia mlo” alibaini mama moja aliyekutwa kwenye soko ya Bubanza.

Madhara : watoto wameanza kuacha shule. Hali kadhalika kwa baadhi ya wanafunzi wa kata ha Matonge kaskazini mwa mji wa Bubanza.

Kwa mjibu wa kiongozi wa kijiji kimoja, takriban watoto 20 waliacha shule.

” Ni kutokana na njaa ambapo wanafunzi hawaendi tena shuleni, hawapati chakula cha kutosha”, alithibitisha.

Matarajio

” Serikali ingeacha nafaka za vyakula kutoka nje ya nchi kuingia Burundi pasina kulipa ushuru wa foroghani”, alipendekeza mfanyabiashara katika soko la makao makuu ya mkoa huo wa magharibi mwa Burundi.

” Hakika mavuno hayakuwa mazuri na hayatoshi kwa chakula cha wananchi ambao idadi inazidi kupanda.
Hali hiyo inathiriwa na ukosefu wa mvua iliyochelewa kunyesha. Serikali ingefungua biashara ya bidhaa za nafaka za chakula na kuwekeza katika sekta hiyo ” alifahamisha mkulima mmoja.

Mfumo wa kutoa mlo shuleni kwa ufadhili wa PAM (Mpango wa chakula duniani) unapatikana katika baadhi ya shule mkoani Bubanza. Kwenye baadhi ya shule, hakuna watoro hadi sasa.

Wananchi wanalalamika kuwa hali ya shirika hilo la umoja wa mataifa kutumia chakula kilichokusanywa ndani ya nchi ilichangia katika kusababisha upunguvu wa nafaka za vyakula (Maharagwe, mchele)

“Mwaka huu ulitangazwa na rais kama mwaka wa kilimo. Licha ya hayo ni mwaka wa mzozo katika upatikanaji wa nafaka za vyakula mkoani Bubanza, ambao ni maarufu katika uzalishaji wa mchele, maharagwe, mihogo na ndizi” alilalamika mfanyakazi wa serikali.
ujanja kuhusiana na upatikanaji wa mbolea za kizungu FOMI, ulisababisha kupungua kwa mavuno ya mpunga, pamoja pia na ukosefu wa maji ya kumwagilia ambao ulisababishwa na kushindwa katika ujenzi wa bwawa la kumwagilia la Kajeke( Mkoa wa Bubanza).

Waakazi wengi wenye umri zaidi ya miaka 50 walitoa ushahidi kuwa ” hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi bei kupanda kwa kiwango hiki na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha”

Previous Beni: deads and burnt houses in an attack by the ADF
Next Kakuma (Kenya): wakimbizi kutoka burundi wameshambuliwa na mmoja alifariki

About author

You might also like

Governance

Burundi : the fuel crisis far from being resolved

After more than 18 months of fuel crisis, the Burundian authorities give no hope. They announce measures which don’t last. Activists themselves, propose that a round table on the issue

Economy

Rumonge : power cuts and load shedding paralyze economic activities

Residents, traders and financial institutions operating in Rumonge (southwest Burundi) say they are recording enormous losses. This is due to the instability of electricity in the province. Regideso, the only

Society

Photo of the week : Burundians go to stock up on fuel in the DRC, the price there is revised upwards

For months, Burundi has been suffering an unprecedented fuel shortage. Some Burundians decide to go look for it in Uvira in the province of South Kivu, in the east of