Kakuma (Kenya): wakimbizi kutoka burundi wameshambuliwa na mmoja alifariki

Kakuma (Kenya): wakimbizi kutoka burundi wameshambuliwa na mmoja alifariki

Kisa hicho kilitokea nyakati tofauti katika kipindi cha chini ya wiki mbili ndani ya kambi ya Kakuma kaskazini magharibi mwa Kenya. Waathiriwa walivamiwa na watu wasiojulikana ambao walimujeruhi mmoja. Waliwapora pia vifaa vyao. Jamii ya warundi ndani ya kambi ya Kakuma wanaomba msaada. HABARI SOS Médias Burundi

Tarehe 29 oktoba mwanaume kwa jina maarufu “Sebabiri” mkaazi wa zone III bloc 4 alipigwa hadi kufariki dunia.
“Alivamiwa na wakimbizi wanaotumia ki lugha cha sudani-kusini katika jamii ya Nuer. Ilikuwa majira ya saa nne za usiku wakati akiwa karibu na nyumbani kwake. Waliomushambulia ni ma afisa wa usalama”, majirani walifahamisha.

Sababu za kisa hicho bado kujulikana.

” Hatujuwi kwa nini aliuwawa. Inasemekana kuwa watu hao waliahidi kulipiza kisasi kwa hoja kuwa mtoto wa marehemu alimubaka msichana kutoka sudani-kusini. Tunasema kuwa ni madai ambayo hayana msingi. Wangepeleka mashtaka kwenye vyombo vya sheria ” waliongeza kusema.
Uchunguzi ulianzishwa, mke wake ni miongoni mwa watuhumiwa.

” Hakika ni jambo lisilokubalika. Mke wake alienda kushtaki kwa polisi na faili ikamurudiria na sasa anafungwa pamoja na watu wengine kumi” wanalaani warundi ambao wanaomba uchunguzi usioegamia upande ufanyike.

Na wikendi iliyopita haikuwa rahisi kwa wakimbizi wengine watatu kutoka burundi ambao walianguka katika mtego wa watu wasiojulikana.

“Wawili kati yao wanaishi ndani ya zone ya Kakuma II bloc 2 na wa tatu ni mkaazi wa Kakuma III. Walijeruhiwa kwa mapanga. Wa kwanza kichwani, wa pili kwenye uso na wa tatu kwenye tako. Waliporwa pesa yao yote. Kitita cha shillingi za Kenya 5000, simu za mkononi, beskeli na vifaa vingine vya thamani. Wavamizi hao pia ni raia kutoka sudani kusini” walisema wakimbizi kutoka burundi.

Warundi hao waliahidi kujichukulia sheria mikononi iwapo viongozi hawataingilia kati. ” Hatuwezi kulea mikono dhidi ya uonevu huo sababu tunaona hatulindwi kamwe” wanasema.

Watetezi wa haki za binadamu wanatoa tahadhari.

CBDH/VICAR, muungano wa watetezi wa haki wakimbizi wanaoishi ndani ya kambi ” wanalaani vikali mwenendo wa wakimbizi kutoka sudani wanaoshambulia wakimbizi wengine”.

” Tunalaani pia kuona uchunguzi unaofanywa na polisi wa Kenya ukichelewa ili kuwafichua na kuwaadhibu wahalifu na hivyo kuwakata nguvu wanaofanya uhalifu hao unaopeleka uhai wa wakimbizi hasa kutoka burundi ” alifahamisha Léopold Sharangabo naibu kiongozi wa CBDH/VICAR.

Muungano huo unaofanyia kazi katika kambi 10 za wakimbizi unaomba serikali ya Kenya “kuhamasisha polisi kuhakikisha usalama katika maeneo yote na kufanya uchunguzi wa ndani kabisa ili wahalifu wakamatwe”.

“kuna kitu nyuma ya visa hivyo sababu ni warundi hasa wanaolengwa.Kwa nini wavamiaji wanalenga jamii moja? Ni swala ambalo polisi ingetakiwa kujibu”, anasema Bwana Sharangabo.

Kakuma inawahifadhi wakimbizi zaidi ya laki mbili kutoka mataifa mbali mbali wakiwemo warundi elfu 20.

Previous Bubanza: idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na njaa yaongezeka
Next Nyanza-Lac: two people seriously injured following a land dispute