Burundi: kampuni ya katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD kutuhumiwa kufanya ushindani usio wa haki

Burundi: kampuni ya katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD kutuhumiwa kufanya ushindani usio wa haki

Wamiliki wa viwanda wengi na walanguzi wanalalamika juu ya ushindani kwenye soko wa kampuni ya Eagle Mineral Water inayouza maji safi. Kampuni hiyo inamilikiwa na Wakfu wa ”Pax Burundi” chini ya uongozi wa Reverien Ndikuriyo katibu mkuu wa chama tawala cha CNDD-FDD. Wanafahamisha kuwa walipewa amri ya kuacha nafasi ya bidhaa ya Eagle Mineral Water. Wengine wanahakikisha kuwa walitishiwa na watu wa idara ya upelelezi (SNR). WABARI SOS Médias Burundi

Wafanyabiashara wanaotengeneza na kuuza maji safi wanalaani kuwa kampuni ya katibu mkuu wa chama tawala aliwaiba wateja.

“Amri ilitolewa na Reverien Ndikuriyo kuwa kila mlanguzi wa maji analazimika kulangua maji ya Eagle Mineral Water mkoani Makamba ( kusini mwa nchi). Mjumbe wa Bwana Ndikuriyo alikuja ndani ya ofisi yangu na kunifikishia ujumbe kuwa ninatakiwa kupunguza uzalishaji wangu wa kila wiki kwa 40% ili Eagle Mineral Water ipate soko. Sio mimi binafsi niliyepata ujumbe huo. Wamiliki wa kampuni zingine za maji walipata vitisho”. alithibitisha B.N*, meneja wa kiwanda Bujumbura (Jiji kuu la biashara) ambaye alipendekeza jina lake lihifadhiwe kuogopa kufuatiliwa.

Hali ni kadhalika kwa walanguzi.

” Niko na soko la maji katika mashirika mengi nchini Burundi. Afisa wa mauzo ndani ya kampuni ya Eagle Mineral Water alinifahamisha kuwa ninalazimika kuuzisha maji ya kampuni hiyo ili niweze kuendelea na soko hilo. Nilijinyamanzia lakini jeshi wa cheo cha juu anayefanyia kazi idara ya upelelezi alinipigia simu na kuniambia kuchagua kati ya kuuzisha maji ya Eagle Mineral Water na kuuwawa. Nilikubali mara moja. Walinitishia kuwa akaunti zangu ndani ya benki zitafungwa iwapo sintakubali amri hiyo” , alifahamisha J.H*

Hali ni kadhalika kwa wamiliki wa hoteli.

Ili kupata wateja na masoko, ni lazima kuheshimu amri kutoka juu ya kutumia maji ya Eagle Mineral Water” alibaini M.B* mfanyakazi kwenye hoteli ya kifahari mjini Bujumbura.

Kufuatia madai hayo, SOS Medias Burundi ilimpigia simu afisa wa mahusiano wa shirika la Pax Burundi ” Alijizuia kuelezea chochote kuhusiana na kesi hiyo.

*Majina ya watu waliozungumza na SOS Medias yamebadilishwa kwa sababu za kiusalama.

Previous Rumonge: economic activities paralyzed, the population forced to welcome the torch of peace
Next Nduta (Tanzania): ghasia kati ya polisi na wakimbizi kutoka Burundi