Nduta (Tanzania): ghasia kati ya polisi na wakimbizi kutoka Burundi

Nduta (Tanzania): ghasia kati ya polisi na wakimbizi kutoka Burundi

Tangu weekendi iliyopita, polisi imekuwa katika harakati za kuwakamata wafanyabiashara wanaoendeshea shughuli zao nyumbani. Maduka pia yanachomwa moto. Hasira ya wakimbizi ilipanda hadi kuwarushia mawe polisi. HCR ilijaribu kutuliza hali. HABARI SOS Médias Burundi

Maeneo yaliyolengwa hasa ni yale ya zone 18, 20 na 21. Polisi ilitafuta bidhaa zilizohifadhiwa nyumbani na ambazo zinaendelea kuuzwa wakati ambapo masoko na maduka vilifungwa tena.
Hasira ilipanda pale ambapo polisi walibomoa nyumba zinazotumiwa kama maduka.

” Walikuwa wanamaliza kubomoa nyumba 10 zikiwemo zile za wajane kwa hoja kwamba walikuta ndani matunda, mboga boga na kreti ya soda kwa ajili ya kuuzisha. Kwa hiyo, hatungendelea kulea mikono. Baadhi yetu waliwarushia mawe askali polisi. Upande wao walitumia gesi ya kutoa machozi ili kutusambaratisha. Pande mbili zilipata majeruhi madogo” alieleza mkimbizi mmoja.

HCR iliingilia kati ili kutuliza hali

” Pasina kushituka , mfanyakazi wa HCR aliwasili na hakulaani visa hivyo vya kubomoa nyumba zilizojengwa na HCR kwa ajili ya wakimbizi. Alituelezea tu tusiwapigi tena mawe askali polisi, tuwaache wafanye kazi yao na tujiepushe kukabiliana nao, jambo linaloonyesha kuwa HCR haina nguvu au ni mshirika” wanalaani raia wa Burundi.

Kuitishwa……

Wakimbizi wengi hasa vijana walisimamishwa. Wanazuiliwa jela.
” Tunaomba HCR kutupilia mbali unyanyasaji unaofanywa dhidi yetu na kuchangia ili raia wenzetu waweze kuachiwa huru. Tuko katika matatizo hapa ndani ya kambi nchini Tanzania” wanazidi kusema wakimbizi kutoka burundi.

Wakimbizi wanadai kuwa ni njama za kuwalazimisha kurudi makwao sababu serikali ya burundi na ile ya Tanzania walikubaliana kuwa wakimbizi wote ni lazima warudi makwao ” kwa hiari au kwa nguvu “.
Wanaomba jamii ya kimataifa na HCR tawi la afrika mashariki kuingilia kati ili kuheshimisha makubaliano kuhusu haki za wakimbizi.

Nduta ndio kambi kubwa ya wakimbizi kutoka Burundi nchini Tanzania, ina zaidi ya wakimbizi elfu 76.

Previous Burundi: kampuni ya katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD kutuhumiwa kufanya ushindani usio wa haki
Next Burundi: a company of the CNDD-FDD party secretary general accused of unfair competition