Bururi : gereza limezidiwa na idadi kubwa ya wafungwa

Bururi : gereza limezidiwa na idadi kubwa ya wafungwa

Gereza la Bururi (kusini mwa Burundi) linawahidhi wafungwa ambao wanazidi uwezo wake kwa mjibu wa vyanzo katika idara ya magereza. Inawapa hifadhi watu 383 wakati uwezo wake hauzidi watu 250. HABARI SOS Médias Burundi

Viongozi wa idara ya magereza wanasema mazingira gerezani ni mabaya. Waziri wa sheria analaani kuona kuna watu wanaozuiliwa jela wakati hawatakiwi kukaa jela. Anaomba mahakama kuwajibika ili kupunguza msongamano katika magereza.

Msongamano katika magereza mkoani Bururi unathibitishwa na vyanzo vya wizara ya sheria, watetezi wa ndani wa haki za binadamu na watu wa karibu ya wafungwa.

” Gereza ambalo lina uwezo wa kuwapokea watu 250 sasa linawapa hifadhi wafungwa 383. Hali hiyo inasababisha mazingira mabaya gerezani, wanasema.

Kulingana na vyanzo, gereza lina wafungwa 117 waliokatiwa kesi, wanaosalia wote bado ni watuhumiwa.

Bururi na katika magereza mengine nchini, msongamano wa wafungwa ni changamoto kubwa ambayo inasababisha hasara kubwa kwa serikali, kulingana wa waziri wa sheria.

“[….] Kuanzia malaazi, chakula na huduma za afya, hayo yote yanagharimu kitita kikubwa serikali […] alifamisha Domine Banyankimbona katika tamko lake la tarehe 31 oktoba.

Anawaomba kujirekebisha wadau wa sheria na majaji wanaosababisha ongezeko la wafungwa magerezani kwa kuwatuma gerezani watu waliofanya ” makosa madogo”.

Domine Banyankimbona anaomba majaji kushughulikia kwa makini faili za makosa madogo na zile za watu ambao kesi zao hazijakatwa.

Previous Bururi: prison house overcrowded
Next Lusenda: Burundian refugees asked not to leave the camp

About author

You might also like

Justice En

Goma: ma mia ya visa vya ubakaji yaripotiwa eneo la Kanyarutchinya

Visa vya unyanyasaji wa kijinsia viliongezeka katika kijiji cha Kanyarutchinya wilayani Nyiragongo na Bulengo magharibi ya mji wa Goma Kivu kaskazini tangu kuibuka tena kwa kundi la M23. Viongozi wa

Human Rights

Burundi: lawyer Tony Germain Nkina acquitted

Burundian lawyer and activist Tony Germain Nkina was acquitted on Tuesday morning. The Ngozi Court of Appeal (Northern Burundi) which cleared him also discharged his co-accused Apollinaire Hitimana. Human Rights

Refugees

Nyarugusu (Tanzania): a concerning showdown between two humanitarian organizations

In the Nyarugusu camp, two humanitarian NGOs compete in the area of ​​education. These are “Save the Children” and “IRC”. As a result, schools did not open on Monday. INFO