Ntega : wanawake tisa waliuwawa na waume zao kwa kipindi cha mwaka mmoja

Ntega : wanawake tisa waliuwawa na waume zao kwa kipindi cha mwaka mmoja

Wakaazi wa tarafa ya Ntega mkoani Kirundo (kaskazini mwa Burundi) waliomba adhabu ya kunyongwa iweze kurudishwa kwa ajili ya kushughulikia watu wote wanaofanya mauwaji. Ombi hilo limejiri baada ya mauwaji ya mwanamke mmoja mkaazi wa kijiji cha Monge, mauwaji yaliyotokea januari tarehe 23. Angalau wanawake tisa waliuwawa na waume zao katika tarafa hiyo kati ya januari 2022 na januari 2023. HABARI SOS Médias Burundi

Katika mkutano wa gavana wa mkoa wa Kirundo siku ya alhamisi iliyopita, wakaazi wa tarafa ya Ntega walijieleza kuhusu visa vya mauwaji vilivyoripotiwa katika miezi iliyopita ndani ya eneo hilo.

Akinama tisa waliuwawa na waume zao tangu mwaka wa 2022. Kisa cha hivi karibuni kilitokea siku ya jumatatu iliyopita. Askali jeshi wa Burundi Pascal Bizimana mwenye cheo cha koporo alimuuwa mkeo.

Mahakama ya mkoa wa Kirundo ilimkatia adhabu ya kifungo cha maisha gerezani. Alitakiwa pia kulipa faini ya franka za Burundi milioni 25 kwa familia ya mkeo kama fidia.

Siku nane badaye, maiti ya mwanamke mwingine kwa jina la Sandrine Nibigira mwenye umri wa miaka takriban 30 iliogotwa. Mume wake ambaye anatuhumiwa mauwaji hayo ya mkeo, alitoroka maeneo ya Musumba ambako alikuwa anaishi. Polisi inafahamisha kuwa iko mbioni kumtafuta. Akimama hao wawili waliouwawa katika mwezi januari wanaongeza idadi ya wengine sita waliouwawa na waume zao pia katika mwaka wa 2022 kwa mjibu wa vyanzo katika utawala.

Wakaazi wa tarafa ya Ntega waliomba ” auwawe mara moja mtu yoyote anayefanya mauwaji”.

Wanasema kusikitika na kuona wahalifu wakiachiliwa huru kutoka jela kutokana na rushwa inayokabili sekta ya sheria.

” Sehemu kubwa ya visa vya uhalifu vinavyofanyika hutokana na hali ya kutoadhibu”, alisisitiza mwanamke mmoja katika viongozi wa tarafa hiyo.

Viongozi wa ndani wanakosoa mfumo wa sheria.

” Mahakama ya Kirundo inakabiliwa na rushwa” alilaani hadharani kiongozi mmoja.

Gavana wa mkoa wa Kirundo Albert Hatungimana anafafanua kuwa adhabu ya kunyongwa haiwezi kutekelezwa. Katiba ya Burundi iliondoa adhabu hiyo.

Asilimia 98 ya wakaazi wa tarafa ya Ntega waliohudhuria mkutano huo walichagua kwa kupandisha mikono irudishwe adhabu ya kuuwawa dhidi ya watu waliotekeleza mauwaji .

Previous Rwanda : HCR yatafuta wakimbizi kwa ajili ya Canada
Next Rwanda-DRC : maafisa wakuu wa Jeshi la Rwanda wanaohudumu katika mashirika ya kikanda wameitishwa