Rwanda : HCR yatafuta wakimbizi kwa ajili ya Canada

Rwanda : HCR yatafuta wakimbizi kwa ajili ya Canada

HCR-Rwanda iko kwenye hatua ya kuhamasisha jamii ya wakimbizi kwa ajili ya kuhamia nchini Canada kwa sababu za kiuchumi. Baada ya Kigali, ni zamu ya kambi ya Mahama. Lengo : Kutafuta wakimbizi wenye uzowefu wa kazi kwa ajili ya kuajiriwa nchini Canada. Ni mradi unaoleta hisia kali kwa sehemu kubwa ya wakimbizi. HABARI SOS Médias Burundi

Siku mbili zilitosha kwa HCR na Minema, wizara ya inayohusika na wakimbizi nchini Rwanda kwa ajili ya kuwafafanulia wakimbizi wa mjini Kigali programu iliyoanzishwa na Canada kuhusu uhamiaji kwa sababu za kiuchumi, ilikuwa mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Walielezea kuwa wakimbizi wenye taaluma fulani ya kazi wanaweza kujaribu bahati yao.

” Walimu, wauguzi, wafundi wa magari, madereva, wahandisi wa kilimo, waliosomea elimu ya kampuita, wandishi wa habari, watalaam katika lishe na chakula, wasanii ……orodha inaweza kuwa ndefu. Mnaweza kupima bahati yenu. Makampuni mengi nchini Canada yanaajiri. Na nchi hiyo imeamuru kupendelea wakimbizi kwa ajili ya visa za bure za uhamiaji kwa ajili ya sababu za kiuchumi” , alielezea mjumbe wa HCR kwa ajili ya kuamsha utashi kwa ma elfu ya wakimbizi ambao sehemu kubwa ni kutoka Burundi na Kongo waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha kijamii cha Gikondo mjini Kigali kwa siku mbili.

Aliwaomba kuweka tayari vyeti vyao kuanzia shahada ya kufuzu elimu ya sekondani na za kiufundi.

HCR inasema iko tayari kusaidia katika hatua ya maombi iwapo itahitajika. ” Lakini tulifafanulia hatua, na karatasi zinazohitajika na tumewaonyesha njia na anuani zote kwa ajili ya kuwasilisha maombi”, HCR na Minema walisikika wakisema.

Alhamisi na siku ya ijumaa ilikuwa zamu ya kambi kuanzia kambi ya Mahama inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi na Kongo kwenye ardhi ya Rwanda.

Utashi, ndoto na ukosefu wa matumaini ……

Mjini Kigali ni mada hiyo peke inayojadiliwa katika jamii ya wakimbizi.

” Walituelezea kuwa ni takriban watu 500 ambao watahamia nchini Canada kupitia programu hiyo. Mimi muhandishi katika elimu ya kompiuta, ninatakiwa kuwa miongoni mwa hao. Acha nitafute habari kuhusu mambo yanayohitajika ili niweze kuwasilisha faili yangu mapema. Pengine ni Mungu aliyetutakia sisi kuacha maisha haya magumu hapa katika jiji la Kigali kama mkimbizi ambaye hana ajira” alielezea JMV mkimbizi na kiongozi wa familia changa

Na kuzidi kusema : ” Hamtaniona tena, ninakaribia kuchukuwa ndege na kwenda ” kama kujipa matumaini, kujihakikishia.

Kwa wengine ni ndoto.
” Mnafikiria kuwa Canada ni fuko la takataka la kupokea wakimbizi hao! Acheni ndoto zenu, itakuwa bahati ya mtu kama inavyokuwa kuhusiana na Green Card ya Marekani. Kwa vyovyote vile, mimi sitaki kupoteza muda wangu”, akidai mkimbizi mmoja.

Hata hivyo, wengine wanachagua kupima bahati yao.

“Mimi, kwanza lilijaribu kwa ajili ya mke wangu ambaye ni muuguzi na faili yake ikipokelewa vizuri, nilisikia kuwa taluuma yake ilipewa kipau mbele. Mimi niko katika sekta ya teknolojia za kisasa, nitaamuru badaye iwapo nitawasilisha maombi”, alisema EM mkimbizi baba wa watoto watatu.

Katika kambi ya Mahama, ni hali ya kupoteza matumaini inayojaa mioyo.

” Kwenye uwanja ambako kampeni hiyo ilitekelezwa, hapakuwa na umati mkubwa. Kwanza kabisa sababu ni kwamba idadi kubwa ni watu ambao hawakusoma. Wengine ni wakimbizi kutoka Kongo ambao mchakato wa kuwahamisha unaendelea. Harafu idadi kubwa ni watu waliopoteza matumaini ambao watataka kurudi makwao”, vyanzo vyetu ndani ya kambi vinahakikisha.

” Hapa tunataka chakula peke yake. Hakuna kitu kingine, sababu njaa inafanya majanga. Harafu walituambia kuwa maombi yaliwasilishwa pia katika nchi zingine. Kwa hiyo bahati ni ndogo”, wanalaani wakimbizi kutoka kambi ya Mahama.

Hata hivyo, HCR na wizara ya wakimbizi pamoja na mashirika mengine ya kiutu yanayowahudumia wakimbizi yanaomba wakimbizi hao kuwasilisha maombi kwa wingi hasa vijana kwa ajili ya kujaribu bahati kupitia programu hiyo ya uhamiaji kwa sababu za kiuchumi nchini Canada.

Kwa wale ambao watachaguliwa, hawatalipa gharama za visa na mchakato wote hadi kununua tiketi ya ndege utakuwa bure” , HCR ilihakikisha.

Previous Ntega : nine women killed by their husbands in one year
Next Ntega : wanawake tisa waliuwawa na waume zao kwa kipindi cha mwaka mmoja