Rwanda-DRC : maafisa wakuu wa Jeshi la Rwanda wanaohudumu katika mashirika ya kikanda wameitishwa

Rwanda-DRC : maafisa wakuu wa Jeshi la Rwanda wanaohudumu katika mashirika ya kikanda wameitishwa

Rwanda imeitisha jumanne hii maafisa wakuu wa jeshi wanaohudumu katika mashirika ya kikanda ambao wako kwenye ardhi ya Kongo. Ni kufuatua hatua ya Kinshasa ya kuwafurusha wale maafisa ambao wanahudumu kwenye uongozi wa kikosi cha EAC mjini Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu-kaskazini (mashariki mwa RDC). Kigali na Kinshasa wanatuhumia uhaini. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa kauli ya msemaji wa jeshi lake, Kinshasa iliamuru kuwafukuza kwenye ardhi yake wanajeshi wakuu wote wa Rwanda wanaohudumu katika kikosi cha kikanda cha EAC kwenye ngome kuu ya kikosi hicho.

” Kwa sababu za usalama wa nchi yetu, tumewaomba maafisa wakuu wa jeshi la Rwanda wanaofanyia kazi mjini Goma katika ngome kuu kurejea makwao” amefahamisha jemedali Sylvain Ekenge.

Baada ya hatua hiyo kutangazwa, Kigali imejibu kwa kuchukuwa hatua ya kuwaitisha maafisa wakuu wa jeshi lake wanaohudumu katika mashirika yote ya kikanda nchini DRC.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, bila hata hivyo kutoa ushahidi, Kinshasa ilidai kuwa kikosi maluum cha jeshi la Rwanda kiliingia nchini Kongo ” kufanya mauwaji ya watutsi wa Kongo ni kupatika harka hiyo kwa jeshi la Kongo kwa ajili ya kupata hoja ya kuelezea sababu za kuwepo kwa jeshi la Rwanda kwenye ardhi ya Kongo”.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili jirani ya kanda ya maziwa makuu ya Afrika unazidi kuzorota. Kinshasa inatuhumu Kigali kuwaunga mkono waasi wa M23, kundi linaloundwa sehemu kubwa na watutsi wa Kongo na ambalo lilichukuwa silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutotekeleza ahadi zake za kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake. Baada ya utulivu wa siku chache, kundi la M23 lilianza tena vita na kusema kuwa linataka kuwalinda raia waliowachache wa Kabila la watutsi dhidi ya mauwaji yaliopangwa na Kinshasa “. Alhamisi iliyopita, kundi hilo lilichukuwa udhibiti wa jiji la Kitshanga kwenye umbali wa kilometa 80 kaskazini magharibi ya mji wa Goma baada ya siku tatu ya mapigano makali.

Katika kikao cha baraza la mawaziri cha mwisho wa wiki, raia Tshisekedi alihakikisha kuwa hatua zote zilichukuliwa ili kufungia njia Rwanda na kundi la kigaidi la M23.

Waangalizi pamoja pia na watetezi wa haki za binadamu wanahofia kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi wakati ambapo tahadhari ya kutokea janga la kibinadamu zikizidi kutolewa. Zaidi la wananchi elfu 60 walitoroka makaazi yao kutokana na mapigano katika wilaya moja ya Masisi kulingana na viongozi wa ndani.

Mashirika ya kiraia ya Kivu kaskazini yanatuhumu kikosi cha kikanda kufanya undumia kuwili kwa kuunga mkono kundi la M23.

Rwanda inatupilia mbali tuhuma za jirani wake wa magharibi huku upande wake ikituhumu Kongo kushirikiana na kundi la FDLR la waliofanya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda kwa kuwapa sare, silaha na risasi kwa ajili ya kuvuruga ardhi yake “. Papa François ambaye ameanza ziara katika nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati jumanne hii, amejizuia kuelekea mjini Goma kama ilivyokuwa kwenye agenda yake kabla. Lakini atawapokea wawakilishi wa waathiriwa wa maovu na vurugu vinavyofanyika mashariki mwa RDC.

Previous Ntega : wanawake tisa waliuwawa na waume zao kwa kipindi cha mwaka mmoja
Next Rumonge: three drink sellers brought to justice