Bujumbura : kwa mara nyingine, wakuu wa nchi za EAC watoa wito wa kusitisha vita mara moja

Bujumbura : kwa mara nyingine, wakuu wa nchi za EAC watoa wito wa kusitisha vita mara moja

Kwa hali isiyo ya kawaida, wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki walikutana jumamosi tarehe 4 februari 2023 jijiji Bujumbura makao makuu ya kibiashara ya Burundi. Hali ya usalama inayojiri nchini Kongo ndio ilikuwa agenda ya kikao hicho kilichohudhuriwa na marais wote wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika isipokuwa tu rais wa Sudani kusini. Kupitia tangazo la kuhitimisha kikoa, iliamuriwa kuwa pande hasimu zinatakiwa kuweka silaha chini na kuanza mazungumzo mara moja. Mkutano huo uligunduwa kuwa swala la hali ya usalama mashariki mwa DRC ni tatizo la ukanda mzima na suluhu la kudumu litapatikana kupitia mchakato wa kisiasa. Mkutano ulisisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha mazungumzo kati ya pande zote. Lakini makundi ya ndani yanatoa masharti kadhaa moja ya masharti hayo ikiwa kufukuzwa kwa makundi ya nje yanayopatikana kwenye ardhi ya kongo”. HABARI SOS Médias Burundi

Ma rais wa nchi wa ukanda huu walilazimisha vita isimame mara moja kwa makundi yote ya silaha yakiwemo ya nje na kuwaamuru wakuu wa majeshi kukutana katika kipindi cha wiki moja na kuonyesha kalenda ya kuondoka kwa waasi na ramani ya kuweka wanajeshi wa jumuiya alifahamisha Peter Mathuki katibu mkuu wa EAC aliyesoma tangazo la kuhitimisha mkutano huo.

Pamoja na hayo, kikao kiliomba mchakato huo ufanyike sambamba na mazungumzo.

” Ukiukwaji ya amri hiyo utafahamishwa mwenyekiti wa kikao kwa ajili ya kuzungumzia mara moja na wajumbe wa kikao”.

“Daima kulingana na tangazo hilo, ma rais waliomba nchi zote zilizoahidi kutuma wanajeshi kufanya hivyo mara moja. Nchi ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ilitolewa wito wa ” kurahisishia wanajeshi kutoka Sudani kusini na Uganda wanaotaka kujiunga na kikosi cha afrika mashariki.

ufadhili
Pointi nyingine muhimu inahusu uchumi. Nchi kama Rwanda, Tanzania, Kenya na Uganda, ziliahidi kuchangia fedha.

Mbali na jamii, pesa nyingi zinatoka katika umoja wa mataifa, umoja wa Afrika, uingeleza na pia Sénégal

Picha ya marais wote haikupigwa

Wakati wa kikao, ma kumi ya wandishi wa habari waliokuwa Ntare House ( ikulu ya rais wa Burundi) walikuwa wamejipanga kwa ajili ya picha ya familia.

Kwa kushitukiza wote, rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliondoka kabla ya sherehe za kuhitimisha.

Watu wote walifikiria kuwa amepata dharura.

Hali iliyosababishwa wasi wasi zaidi ni pale rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni alipoondoka dakika chache badaye.

“kutofautiana ! Hii ni dalili mbaya . Oh! Kongo yangu masikini” alisikika akisema kwa sauti ya chini mwandishi wa habari mmoja kati ya wajumbe kutoka Kongo.

Familia ya ma rais ilikuwa haienei, picha iliyokuwa imepangwa kupigwa huku mabango ya nembo ya kila nchi yakiwa yaliwekwa kuonyesha nafasi ya kusimama kwa kila rais kati ya hao saba, haikupigwa.

Tangazo la kuhitimisha kikao lilisomwa hiyo hiyo siku jioni.

Kagame alikuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa nchini Burundi

Mara ya mwisho warundi kumuona rais Kagame katika nchi yao ni kwa kipindi cha karibu miaka 10 iliyopita. Burundi na Rwanda nchi hizo jirani hivi karibuni zilianza kuimarisha uhusiano uliozorota tangu mwaka wa 2015. Kando na mkutano huo na mamkizi kati ya rais Ndayishimiye na Paul Kagame yaliyokuwa na maana kubwa, marais hao wawili walikutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana.

Licha ya ofisi zao za mawasiliano kuamuru kutoangazia mazungumzo yao, idadi kubwa ya waangalizi wanadai kuwa inaonekana rais Ndayishimiye alirejelea ombi la viongozi wa Burundi kwa mwenzake wa Rwanda ” la kuwarejesha watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake lililofeli katika mwezi mei 2015 ili washughulikiwe na vyombo vya sheria nchini Burundi”.

” Bila shaka rais Kagame alimuomba rais wa Burundi kuwakataza baadhi ya washirika wake kuacha kushirikiana na kundi la FDLR waasi wa Rwanda waliofanya mauwaji ya kimbari na kuzuia nchi yake kutumiwa kama kama njia kwa wajumbe wa kundi hilo linalopigana dhidi ya utawala wa Kigali ambao walipiga kambi katika mkoa wa Kivu ya kusini”, anadai mwandishi wa habari mtalaam wa maswala ya maziwa makuu .

Majibu ya makundi ya silaha

Baadhi ya makundi ya silaha yalitoa majibu kuhusiana na maagizo ya mkutano huo wa Bujumbura. Mfano ni kundi la Mai Mai Biloze Bishambuke.

” Ni lazima kwanza makundi ya nje ya nchi yarudi katika nchi zao za asili hususan kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda, Red Tabara, FDLR, Imbonerakure, FNL, Forebu, CNRD……sababu hakuna kundi hata moja la kujihami ambalo linapatikana nchini Rwanda, Burundi, Uganda na kuvuruga usalama wa nchi hizo “, alibaini Aimable Nabulizi, msemaji wa kundi la Mai Mai Biloze Bishambuke.

Kwa mjibu wa kundi hilo linalodai kuwa ni kundi la kuwalinda wananchi, maeneo yasiodhibitiwa katika mkoa wa Kivu kaskazini yanatakiwa kuondolewa.

” Iwapo EAC ilikuja kusaidia FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) inatakiwa kwenda uwanjani kushambulia kundi la M23, kinyume chake kikosi hicho cha kikanda kinatakiwa kuondolewa nchini DRC kwa sababu kinapendelea upande wa M23″, anadai Nabulizi ambaye anatuhumu pia nchi za Rwanda na Uganda kuunga mkono kundi la M23. Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo kwamba inaunga mkono kundi hilo la zamani la watutsi lililochukuwa silaha tena mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa kutotekeleza ahadi zake za kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake.

Tshisekedi apaza sauti

Katika video, rais wa Kongo Félix Tshisekedi alionekana akiongea na rais wa Kenya William Ruto na kamanda wa kikosi cha kikanda meja jemedali Jeff Nyagah mwenye asili ya Kenya.

” Hamkuja iki kupendelea kundi la M23 na inasikitisha kuona raia wakiwashambulia. Mulikuja kutusaidia, hamukuja kupata matatizo. Kuweni makini kwa hilo, kuweni wakini, karibu kuyajibu maswala ya wananchi, wasiliana na wananchi ” , alisisitiza rais wa Kenya kwa sauti kali.

Kikosi cha kikanda kilianzishwa na wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki mwishoni mwa juni 2022. Kinakosolewa vikali na mashirika ya kiraia, wanasiasa, viongozi na makundi mengi ya raia wa Kongo wanaodai kuwa ni ” mshirika wa kundi hilo”. Kikosi hicho kinatuhumiwa kutoshambulia M23 na kusalia kati kati”.

Hivi karibuni, watu wengi wakiwemo wandishi wa habari walijeruhiwa ndani ya mji wa Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini wakiwa ndani ya mandamano dhidi ya kikosi hicho.

Kulingana na wandishi wa habari wa ndani, mandamano kama hayo yanapangwa kufanyika jumatatu hii katika mji mkubwa zaidi wa mashariki mwa Kongo.

Jumapili hii, vijana wengi wameteremka katika barabara za mji wa Goma na kufunga barabara moja kudhihirisha upinzani dhidi ya maamuzi ya mkutano wa Bujumbura”.

“Jumatatu hii, mandamano makubwa yanapangwa kufanyika ” gazeti la ndani limefahamisha.

Polisi ilifungua barabara hiyo kwa mjibu wa chanzo cha ndani.

Katika ziara yake ya hivi karibuni mjini Kinshasa, Papa François alitoa wito wa kusitisha vurugu mashariki mwa Kongo na kutuhumu jamii ya kimataifa kama ilijiuzulu kuhusu kushughulikia vurugu zinazowameza raia wa Kongo”. Papa mtakatifu alikutana na wahanga wa maovu yanayotendeka mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati na kuwaambia ” Maumivu yenu ni yangu pia”.

Previous Mzozo mashariki mwa Kongo : askali mmoja wa kikosi cha umoja wa mataifa auwawa na mwingine kujeruhiwa vikali kutokana na shambulizi dhidi ya ndege la Monusco
Next Bujumbura: EAC heads of state call again for an immediate ceasefire in eastern Congo