Mzozo mashariki mwa Kongo : askali mmoja wa kikosi cha umoja wa mataifa auwawa na mwingine kujeruhiwa vikali kutokana na shambulizi dhidi ya ndege la Monusco

Mzozo mashariki mwa Kongo : askali mmoja wa kikosi cha umoja wa mataifa auwawa na mwingine kujeruhiwa vikali kutokana na shambulizi dhidi ya ndege la Monusco

Monusco (ujumbe wa umoja wa mataifa nchini DRC) umetangaza kifo cha askali wake kupitia tangazo. Ujumbe huo unafahamisha kuwa alifariki kutokana na shambulio dhidi ya moja kati ya ndege zake za helikopta ndani ya Kivu kaskazini. Mwingine alijeruhiwa vikali. HABARI SOS Médias Burundi

Monosco inaghadabishwa na kifo cha askali wake kutokana na shambulizi dhidi ya moja kati ya helikopta zake ndani ya mkoa wa Kivu-kaskazini, ujumbe huo wa umoja wa mataifa nchini Kongo umefahamisha jumapili hii jioni.

” Helikopta ya Monusco iliotoka Beni jumapili hii adhuhuri ikielekea Goma imepigwa risasi zilizosababisha kifo cha mmoja kati ya rubani wake na kumujeruhi vikali askali mwingine wa umoja wa mataifa. Ndege hiyo imefanikiwa kutuwa kwenye uwanja wa ndege wa Goma”, ujumbe wa umoja wa mataifa umefahamisha kupitia tangazo.

Bila kutaja uraia wake, Monusco imetoa ” salamu za rambi rambi kwa familia ya muhanga na nchi yake ya asili na kumutakia kupona haraka aliyepata majeraha.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini DRC amelaani shambulio hilo. Bintou Keita amesema ni shambulio la “kijinga ” dhidi ya ndege yenye nembo ya umoja wa mataifa.

Licha ya kuwa ujumbe huo wa UN unaokosolewa vikali haukufahamisha nchi ya asili ya muhanga huyo aliyeuwawa tarehe 5 februari 2023, televisheni ya marekani ya NBC imefamisha kuwa alikuwa mjumbe wa kikosi kutoka afrika ya kusini.

” Mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa umoja wa mataifa yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu wa kivita”, alikumbusha Bintou Keita ambaye anahakikisha kuwa ” waliofanya kitendo hicho cha aibu wanatakiwa kupelekwa mahakama”.

Shambulio dhidi ya ndege hiyo ya Monusco limefanyika katika kitongoji cha Rusayo katika wilaya ya Nyiragongo. Ni kwenye umbali wa kilometa mbili kaskazini ya mji wa Goma, makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa Kongo.

” Eneo hilo linadhibitiwa na FARDC ( jeshi la Kongo) lakini wajumbe wengi wa FDLR wanajificha eneo hilo , vinasema vyanzo vya ndani.

Tukio hilo limejiri masaa 24 baada ya kikao kisicho cha kawaida cha wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki kuhusu hali ya usalama nchini Kongo. Mkutano huo ulifanyika jumamosi hii katika jiji kuu la kibiashara la Bujumbura nchini Burundi.

Viongozi wa EAC kwa mara nyingine waliomba vurugu zisimame na kutoa wito wa kusitisha vita mara moja.

Previous Crise dans l'Est du Congo : un casque bleu tué et un autre gravement blessé dans une attaque contre un avion de la Monusco
Next Bujumbura : kwa mara nyingine, wakuu wa nchi za EAC watoa wito wa kusitisha vita mara moja