Kirundo: mtu aliyerejea kutoka uhamishoni auwawa na wanajeshi

Kirundo: mtu aliyerejea kutoka uhamishoni auwawa na wanajeshi

Mwanaume mmoja aliuwawa na wanajeshi siku ya jumamosi iliyopita alasiri. Kisa hicho kilitokea katika msitu wa hifadhi wa Murehe karibu na mpaka kati ya Burundi na Rwanda tarafani Busoni mkoa wa Kirundo (Kaskazini mwa Burundi). Mhanga huyo ni mwanachi aliyerejea kutoka kambi ya wakimbizi ya Mahama nchini Rwanda, alikamatwa akiwa kwenye makao makuu ya mkoa wa Kirundo akiwa na sihala moja ambayo alificha ndani ya begi iliyojaa mkaa. Alipelekwa badaye katika msitu huo ambako alimaliziwa maisha. HABARI SOS Médias Burundi

Ferdinand Kambayingwe mwenye umri takriban 40 alikuwa mzaliwa wa kijiji cha Kanyinya katika tarafa na mkoa wa Kirundo.

Kulingana na vyanzo kutoka viongozi tawala, Kambayirwe alikuwa amerejea kutoka kambi ya ya wakimbizi ya Mahama mwaka uliyopita.

Vyanzo hivyo vinazidi kuwa alikamatwa jumamosi asubuhi. Kwenye beskeli yake, alikuwa na mfuko uliyojaa mkaa na ambao ndani yake, kulikuwa silaha aina ya AK-47.

Baada ya kushakiwa na wanajeshi wa kambi ya Mutwenzi ( karibu na makuu ya mkoa), alisimamishwa na wanajeshi hao ambao walimulazimisha kuweka chini mfuko huo na kuwaonyesha vitu vilivyokuwa ndani ya mfuko huo.

«Walikuta ndani yake silaha iliyofichwa ndani ya begi », chanzo kutoka katika walinda usalama kilifahamisha.

Mwanaume huyo alifahamisha kuna silaha zingine na risasi vilivyofichwa ndani ya msitu wa Murehe karibu na mpaka bain aya Burundi na Rwanda, kulingana na vyanzo karibu na faili hiyo.

«Alichapwa vya kutosha ili kukubali kisichokubalika kinyume chake hakuwa na silaha nyingine iliyofichwa », alifahamisha askali polisi mmoja ambaye alitaka jina lake lihifadhiwe.

Mara baada ya kuwasili katika katika msitu huo, mwanaume huyo hakuonyesha silaha zingine na risasi kama alivyokuwa ameahidi chini ya manyanyaso. Alijaribu kukimbia na wanajeshi wakampiga risasi », askali polisi mmoja alifahamisha.

Muili ya marehemu ulizikwa mara moja katika tarafa ya Busoni badala ya kuupeleka tarafani Kirundo kwa ajili ya kuzikwa na familia yake.

« Viongozi tarafani Busoni kwa ushirikiano na wale wa taraf aya Kirundo waliharakisha mazishi yake. Hali hiyo iliibuwa wasi wasi baada ya kitendo hicho cha kusikitisha», alihakikisha mteule mmoja kwenye kijiji cha Busoni.

Mkimbizi huyo aliyerejea alikimbilia nchini Rwanda mwaka wa 2015 wakati wa mgogogo wa kisiasa ulioanzishwa na muhula wa tatu wa hayati Pierre Nkurunziza. Familia yake inaomba ukweli kuhusu kifo hicho ujulikane. Wanapendekeza uchunguzi huru uweze kufanyika.

Previous Burundi: vyombo vya habari vya kibinafsi vyakabiliwa na ukosefu wa uwezo wa kifedha
Next Burundi: private media increasingly faced with financial problems