Burundi: vyombo vya habari vya kibinafsi vyakabiliwa na ukosefu wa uwezo wa kifedha

Burundi: vyombo vya habari vya kibinafsi vyakabiliwa na ukosefu wa uwezo wa kifedha

Vyombo vya habari nchini Burundi vinakabiliwa na ukosefu wa uwezo wa kifedha tangu kipindi kilichopita. Idadi kubwa vinawaajiri na kwa muda mrefu wandishi wanaofanya kozi na wengine wa kijitolea ambao hawaombi mshahara mkubwa. Hata na wandishi wa habari wengine wenye mikataba hawapati mshahara wao kwa wakati unaofaa. Fuko la kuunga mkono vyombo vya habari linalopangwa na sheria juu ya uandishi wa habari bado halipo. HABARI SOS Médias Burundi

Tangu mzozo wa 2015, vyombo vya habari nchini Burundi vinafanya kazi kwa kuyumba yumba. Ikiwa vyombo vya zamani na hivi vipya, vyote vinakabiliwa na uhaba wa fedha za matumizi. Ni vichache vinavyoweza kuwalipa mishahara kwa wakati wafanyakazi wake .

« Si jambo la kushangaza kumaliza miezi mitatu pasina kupewa mshahara. Tunafanya kazi kwa kutegemea hali nzuri ya badaye lakini maisha yanaendelea kuwa magumu siku baada ya siku » , alitoa ushuhuda mmoja kati ya wandishi wa habari wa mda mrefu kwenye kituo cha kujitegemea.

Kwa mjibu wa vyanzo vyetu katika vyombo vya habari vingi, baadhi ya waajiri wanawapa kazi wale wanaohitaji kufanya kozi pamoja na wandishi wa kijitolea ambao hawalipwi mshahara ili waweze kuendelea kupeperusha.

Baadhi ya wafanyakazi wanaweza kumaliza miaka miwili wakiwa kwenye hadhi ya yule anayejifundisha kazi au anayejitolea. Hali hii inasababisha watu kuacha kazi, wafanyakazi hao wakijaribu kutafuta mazingira mazuri ya kazi .

Hali hiyo inawaathiri wandishi wa habari. Katika makundi yao ya kujadili kuhusu hali yao, wandishi wa habari bado wanaendelea kuhofia hatma ya taaluma hiyo.

« Uandishi wa habari wa kitaaluma unaendelea kuachia nafasi uandishi wa kujitafutia chakula ambapo ma ripota wanatoa kipao mbele kwa yule anayewapa pesa chini ya majina tofauti (Nauli, pesa ya kupunguza kiwi….. Ni wachache wanaojihusisha na kutengeneza habari zinazowaomba kuwasili uwanjani kwa sababu hawapati pesa» analalamika mmoja kati ya wenzetu.

Kuhusu ufadhili ya vyombo vya habari… ?

Kwa mjibu wa vyanzo ndani ya baadhi ya vyombo vya habari, baadhi ya vituo hunufaika na miradi midogo midogo inayofadhiliwa na wahisani wa ndani hasa.

Lakini mahitaji ya vyombo vya habari ni makubwa kwa kiwango ambapo ufadhili huo hauwezi kumudu mahitaji yote. Idadi kubwa na vyambo vya habari havipati ufadhili wa moja kwa moja wa miradi mikubwa kutoka kwa wafadhili wakubwa( Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi na Uswisi,…..).

« Ufadhili huo unatolewa kupitia shirika la kihisani la Benevolencia », vinasema vyanzo vyetu.

Wandishi wa habari wengi wanakiri kuwa wanaanza kushindwa. Baadhi tayari waliacha kazi hiyo sababu haiwezi kuwawezesha kumudu maisha.

« Walikuwa wananilipa laki moja kwa mwezi. Kutokana na kupanda bei kwa nafaka za vyakula na ughali wa maisha, niliamuru kuacha taaluma hiyo. Bora kwenda kulima katika ardhi yake ndogo », analalamika ripota mmoja ambaye hata hivyo anapenda taaluma ya uandishi wa habari.

« Nikipata bahati ya kumpata muajiri ambaye atanilipa pesa ya kutosha, nitarudi. Ninakumbuka taaluma hiyo », alibaini.

Wiki iliyopita, makamu wa rais Prosper Bazombanza alihakikisha kuwa uhaba wa fedha za kutumia unavikabili vyombo vya habari unachangia pakubwa katika mdororo wa viwango vya taaluma ya uandishi wa habari nchini Burundi.

« Ili kukabiliana na hali hiyo, baadhi ya radio na televisheni huajiri miongoni mwa vijana wasiokuwa na ajira na ambao hawana uzowefu na hali hiyo ilizorotesha taaluma hiyo na kurudisha nyuma uwajibikaji kitaaluma ambao ungetakiwa kutambulisha kazi ya uwandishi wa habari » , alilalamika Bwana Bazombanza.

« Hali itaendelea kuwa mbaya zaidi katika nchi hiyo ambao pesa kutoka matangazo ya biashara ni ndogo na ambapo wandishi wa habari wanaendelea kuzungumzia matatizo yanayoshuhudiwa katika sekta zingine huku wakiamuru kujifanya kama mashujaa wakati ambapo taaluma yao hakika ikizidi kudidimia », anaeleza mwenzetu mmoja.

Sheria ya uwandishi wa habari katika nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki inapanga uundwaji wa fuko la kuunga mkono vyombo vya habari. Bado linabakia ni ndoto licha ya viongozi wa Burundi kuahidi kuwa litaundwa.

Previous Kirundo: a returnee executed by soldiers
Next Kirundo: mtu aliyerejea kutoka uhamishoni auwawa na wanajeshi