Kivu-kaskazini : Mpatanishi Kenyatta ziarani eneo la vita

Kivu-kaskazini : Mpatanishi Kenyatta ziarani eneo la vita

Katika shabaha ya jukumu lake alilopewa na jumuiya ya afrika mashariki, rais huyo mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta jumanne hii amekuwa mjini Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki mwa DRC. Katika ziara hiyo alijipa jukumu la kuwafariji wakimbizi wa vita waliokimbia ujio wa M23 katika eneo la Rutshuru. HABARI SOS Médias Burundi

Uhuru Kenyatta alipokelewa na gavana mwanajeshi wa Kivu-kaskazini luteni jemedali Constant Ndima na kamati yake ya usalama. Wote kwa pamoja walijielekeza kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kanyaruchinya katika wilaya ya Nyiragongo ambayo inawapa hifadhi wakimbizi wa vita laki mbili waliotoroka ujio wa waasi wa M23 inayodhibiti eneo kubwa la Rutshuru.

Katika mkutano na wandishi wa habari, Bwana Kenyatta alisema kuwa anahofia janga la kibinadamu kutokea katika eneo la Nyiragongo ambako kuna ma mia ya wakimbizi.

” Kile nilichoona Goma na maeneo yake ya karibu kinasikitisha. Ni janga la kibinadamu linaloweza kutokea iwapo hakuna kitakachofanyika ” amebaini.

Uhuru Kenyatta aliyechaguliwa mwezi juni na marais wenzake kuwa mpatanishi katika mzozo nchini Kongo, aliwasili mjini Kinshasa (makao makuu ya DRC) jumamosi iliyopita. Tayari alikutana na ma wakuu wa mabaraza mawili ya bunge na seneti vya Kongo na wajumbe wa jamii zenye asili ya mikoa ya Kivu-kaskazini, kivu-kusini na Ituri pamoja pia na wawakilishi wa nchi zao.

Upande wa Kongo ulikariri daima tuhuma zake dhidi ya Rwanda ambayo wanasema kuwa inaunga mkono M23 madai rais wa Paul Kagame kwa mara nyingine wekendi iliyopita aliyakanusha akiwa katika mkutano na shirika la “Unity club ” jukwa la viongozi wa Rwanda lililoanzishwa na mke wa rais Jeanette Kagame.

Previous North Kivu: facilitator Kenyatta visits the combat zone
Next Burundi: msongamano gerezani wakaribia asilimia 200 (waziri wa sheria)