Burundi: msongamano gerezani wakaribia asilimia 200 (waziri wa sheria)

Burundi: msongamano gerezani wakaribia asilimia 200 (waziri wa sheria)

Waziri wa sheria yuko ziarani katika mikoa mbali mbali ya Burundi. Waziri Domine Banyankimbona analaani mwenendo wa majaji wanaowatuma watu gerezani kwa makosa madogo. Anasikitika kuona nchini Burundi ” kuwafunga watu limekuwa jambo la kawaida wakati malaha pengine likiwa jambo la dharura”. HABARI SOS Médias Burundi

Mikoa yote, ujumbe ni ule ule: Jiepushe na kutuma watu ndani ya jela kwa makosa madogo.

Waziri Banyankimbona anahakikisha kuwa katika vikao vya baraza la mawaziri ilidhihirika kuwa ” watu wanasumbuliwa na visa vya wafanyakazi wa sekta ya sheria, majaji na mahakimu”.
Anapokea malalamiko na mashtaka ya wananchi.

Domine Banyankimbona anaomba majaji ” kuandaa mkakati wa kuwaepusha kuchukuwa hatua zinazoegamia upande”. Kuhusu visa vya ubakaji, waziri anakuwa mkali.

” Hatuwezi kucheza na visa vya ubakaji. Iwapo mtaendelea kuwaachilia huru waliofanya ubakaji, kesho au kesho kutwa, wajukuu wetu watakumbwa na visa vya unyanyasaji kijinsia”, alisisitiza akiwa mkoani Cibitoke ( kaskazini-magharibi mwa nchi) baada ya kupata taarifa kuhusu mbakaji aliyeachiliwa huru baada ya miezi miwili ya kifungo peke. Mama wa muhanga ( mtoto wa miaka mitano) anasema ana wasiwasi.

Msongamano gerezani

Kulingana na waziri wa sheria, idadi kubwa ya wale wanaozuiliwa jela, wangetakiwa kuwa huru.

” Tunaweza kuendelea aje ? Tunatuma watu jela pasina sababu. Haitakiwi kuwa hivyo ” , alisisitiza.
Na kulaani kuwa ” kufunga watu jela limekuwa jambo la msingi. Mahala pengine ni dharura”. Kulingana na shirika la akinamama na wasichana kwa ajili ya amani na usalama, wengi wao wanakufa njaa, hawana mahala tosha pa kulala, na hawana huduma za matibabu. Shirika hilo linadai kuwa ” majaji wangetakiwa kuheshimu kanuni na taratibu na kufanya tathmini ya kutosha kabla ya kukata kesi”.

Jeanne d’Arc Zaninyama kiongozi mtendaji wa shirika hilo anaomba wizara ya sheria ” kuchukuwa hatua zinazostahili kumaliza hali hiyo, kuliko kuendelea na matamshi”.
” Lakini anayoyasema waziri ni ukweli” anathibitisha.

Kulingana na takwimu za mashirika ya kutetea haki za wafungwa na kutoka idara ya magereza, ndani ya magereza 11 ya nchi hiyo ya afrika mashariki, kuna mahabusu 13.000 wakati ambapo uwezo wa kupokea wafungwa ni wa 4.149 peke .

Previous Kivu-kaskazini : Mpatanishi Kenyatta ziarani eneo la vita
Next Burundi : a woman takes on the role of ombudsman for the first time