Rutana: mfungwa alifumaniwa akifanya mapenzi, Mwendeshamashtaka aomba pesa wafungwa

Rutana: mfungwa alifumaniwa akifanya mapenzi, Mwendeshamashtaka aomba pesa wafungwa

Wafungwa walilazimishwa kulipa kila mmoja franka elfu 20. Ni pesa iliyokusanywa ili kumlipa asivunje siri mwendeshamashtaka wa Rutana (kusini mashariki mwa Burundi). Mwendeshamashtaka alimufumania mfungwa mmoja akifanya mapenzi katika ofisi ya gereza na msichana wa nje ya gereza. Mfanyakazi huyo wa serikali alilazimisha kupewa pesa ili asilifanyi jambo kubwa. Wafungwa wanaona kuwa ukusanyaji wa pesa hiyo ni “kinyume cha sheria”. HABARI SOS Médias Burundi

Kisa hicho kilifanyika jumapili iliyopita wakati ambapo mfungwa kwa jina maarufu Jegeza alifumaniwa na mwendeshamashtaka wa jamuhuri mkoani Rutana akifanya mapenzi na msichana mmoja ndani ya ofisi ya uongozi wa gereza hilo.
Kwa mjibu wa vyanzo karibu na gereza hilo , mwendeshamashtaka huenda alipewa taarifa na wafanyakazi wa gerezani.
Msichana huyo alipelewa katika jela la kamishena ya polisi tarafa ya Rutana huku mfungwa huyo akirudishwa ndani ya jela.

Siku mbili badaye, mshichana huyo aliachiliwa huru baada ya kutoa hongo kwa mjibu wa vyanzo vya karibu na kamishena ya polisi mkoani Rutana.

Kulingana na vyanzo miongoni mwa wafanyakazi wa gerezani, kiongozi wa gereza aliwatuhumu wafungwa kutoa taarifa za kisa hicho kwa mwendeshamashtaka.
Jumanne hii, mkuu wa gereza kwa ushirikiano na wawakilishi wa wafungwa waliwalazimisha wafungwa wote kulipa pesa franka elfu 20.
Wafungwa ambao hawakupa pesa hiyo walinyanganywa vifaa vyao zikiwemo nguo.
Takriban milioni 10 ndio pesa iliyokusanywa katika zoezi hilo kulingana na vyanzo vyetu.
Wafungwa na familia zao wanaeleza kuwa walilazimika kuuza kuku na mbuzi wao ili kuweza kurudishiwa vifaa vyao walivyokamatwa.
Wafanyakazi magerezani wanamtuhumu kiongozi wa gereza kuwapa nafasi wafungwa wanaotaka kufanya tendo la ndoa kwa sharti la kulipa kitita cha laki tatu na nusu ili kukodi ofisi yake na kuitumbia kama chumba.
Wafungwa wanasema kuwa mara nyingi wamekuwa wanaathiriwa na zoezi hilo la kukusanya pesa kinyume cha sheria. Wanaomba uongozi wa juu wa magereza ” kukomesha unyanyasaji huo dhidi yao” .
Mwendeshamashtaka wa Rutana na kiongozi wa gereza hawakupatika ili kujieleza juu ya madai hayo.

Previous Rutana: a prisoner was caught during sexual intercourses, the prosecutor rounds up prison
Next Rwanda-DRC: mwanajeshi wa Kongo wa pili kuuwawa na jeshi la Rwanda