Gitega: wapinzani wawili wazuiliwa jela kwa zaidi ya mwezi

Gitega: wapinzani wawili wazuiliwa jela kwa zaidi ya mwezi

Wafuasi wawili wa chama cha CNL wa tarafa ya Bugendana mkoa wa Gitega (kati kati ya Burundi) wanazuiliwa jela kwa zaidi ya mwezi mmoja. Wanatuhumiwa kumubaka na kumuuwa mwanamke mmoja. Watuhumiwa wanakanusha madai hayo. Chama chao kinaomba waachiliwe huru. HABARI SOS Médias Burundi

Jonas Nsabimana na Jacques Habonimana, wawili hao wote wafuasi wa chama cha CNL walikamatwa tarehe 12 oktoba iliyopita nyumbani kwao. Walikamatwa na polisi.

Kisa hicho kilitokea katika kijiji cha Nyakeru tarafa ya Bugendana mkoa wa Gitega. Hayo ni baada ya kupatikana kwa muili wa Domine Ngendakumana mwenye umri wa miaka 37 mama wa watoto wawili.
Habari hiyo inathibitishwa na Epimac Mugisha kiongozi wa chama cha CNL tarafani Bugendana ambaye anazidi kuwa muathiriwa huyo aliuwawa baada ya kubakwa. Anatuhumu lakini kijana Imbonerakure ambaye alichangia kinywaji na muhanga huyo katika siku ya kuuwawa kwake.

Domine Ngendakumana na mfuasi huyo wa tawi la vijana wafuasi wa CNDD-FDD walitoka katika mgahawa huo wakiwa pamoja na kuelekea eneo moja, alisema.

Bwana Mugisha anahakikisha kuwa wafuasi hao wawili wa chama cha CNL hawana hatia.

” Walikamatwa kwa ushawishi wa mkuu wa kijiji cha Nyakeru kutokana na kuwa ni wafuasi wa CNL” anazidi kusema.
Anaomba waachiliwe huru.

Mkuu wa kijiji cha Nyakeru Juvenal Butoyi anakanusha madai hayo dhidi yake na kuongeza kuwa wapinzani hao walisimamishwa kwa ajili ya uchunguzi unaoendelea.

Wafuasi hao wawili wa chama kikuu cha upinzani wanazuiliwa kwa sasa ndani ya gereza kuu la Gitega (jiji kuu la kisiasa)

Previous Ituri and North Kivu: at least 18 civilians killed since Sunday
Next Burundi: makamu wa rais anathibitisha uwepo wa uhusiano mbaya kati ya viongozi wa nchi na wandishi wa habari