Burundi: makamu wa rais anathibitisha uwepo wa uhusiano mbaya kati ya viongozi wa nchi na wandishi wa habari

Burundi: makamu wa rais anathibitisha uwepo wa uhusiano mbaya kati ya viongozi wa nchi na wandishi wa habari

Prosper Bazombanza alibaini hayo alhamisi hii kando na kongamano kuu la vyombo vya habari. Alilaani kuwa kazi ya uwandishi wa habari inakabiliwa na hali kushirikisha watu wasiokuwa na uzowefu. HABARI SOS Médias Burundi

Wawakilishi wa serikali, mashirika ya kiraia, wajumbe wa vyama vya kisiasa, mashirika ya umoja wa mataifa, mabalozi na wandishi wa habari walishiriki mkutano huo wa siku mbili katika jiji kuu la kisiasa la Gitega.
Ni makamu wa rais Prosper Bazombanza aliyezindua mkutano huo. Alifahamisha kuwa kuna uhusiano mbaya kati viongozi wa nchi na wandishi wa habari.

” Taaluma ya uandishi wa habari ilishuhudia changamoto na mafanikio katika miezi hii sita iliyopita, na lazima tukubali hilo”, alithibitisha Prosper Bazombanza akikosoa ” baadhi ya wandishi wa habari ambao anasema walibadili muelekeo na kujihusisha na kutaka kufika kwenye utawala kupitia njia isiyokuwa ya kidemokrasia”.

” Hali hiyo inasababisha uhusiano mbaya kati viongozi na wandishi wa habari”, alihakikisha makamu wa rais.

Muakilishi wa shirika la umoja wa ulaya upande wake anakiri kuwa bado wandishi wa habari nchini Burundi wanakabiliwa na vitisho.

[…]Ningetaka kupongeza wandishi wa habari nchini Burundi wa ushuja wao kwa kuendelea kufanya kazi katika hali ngumu na kukabiliwa na vitisho na shinikizo mbali mbali” alifahamisha Claude Bochu. Anazidi kuwa “wandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira magumu na mishahara yao ni midogo”.

Kulingana na makamu wa rais, mazingira hayo magumu yanaathiri uwajibikaji.

” Kufuatia tatizo la ukosefu wa fedha za matumizi baadhi ya radio na televisheni hutafuta wafanyakazi katika vijana wasiokuwa na ajira na ambao hawana pia uzowefu. Hali hiyo ilisababisha taaluma ya uandishi wa habari kurudi nyuma na uwajibikaji unaotakiwa kwa mwandishi wa habari kupotea” alizidi kusema bwana Bazombanza.

Viongozi wa shirika linalojumulusha vituo vya radio (ABR) Onesime Harubuntu anataraji kuwa mkutano huo uliofanyika mkoani Gitega jiji kuu la kisiasa utakuwa ” mwanzo mpya ” . Hii ni baada ya takriban miaka 12 taifa hilo ndogo la afrika likiwa bado halijandaa kongamano kuu la vyombo vya habari.

Previous Gitega: wapinzani wawili wazuiliwa jela kwa zaidi ya mwezi
Next Burundi: the ICC wants to take the next step