Rumonge: mkuu wa tarafa ya Rumonge amukuta mwenzake wa tarafa ya Buyengero gerezani

Rumonge: mkuu wa tarafa ya Rumonge amukuta mwenzake wa tarafa ya Buyengero gerezani

Jérémie Bizimana mkuu wa tarafa ya Rumonge mkoa wa Rumonge (Kusini-magharibi mwa Burundi) sasa ni yuko katika gereza la Murembwe tangu ijumaa. Alimkuta jela mwenzake wa tarafa ya Buyengero pamoja na mshahuri wa gavana anayehusika na fedha na utawala. Wanazuiliwa kwa kosa moja: ubadilifu na wizi wa mabati na mifuko ya simenti vilivyotolewa na ofisi ya rais kwa ajili ya ujenzi wa shule. HABARI SOS Médias Burundi

Jérémie Bizimana alihojiwa na mwendeshamashtaka mkuu wa mahakama ya rufaa mkoa wa Bururi( kusini mwa Burundi) siku ya ijumaa.

Baada ya mahojiano, mwendeshamashtaka aliamuru apelekwe kwenye gereza kuu la Murembwe kwenye kijiji cha Gatete tarafa na mkoa wa Rumonge kusini magharibi mwa Burundi.
Bwana Bizimana amekuwa mkuu wa tarafa wa pili mkoani Rumonge kupelekwa jela katika kipindi cha siku mbili.

Gratien Nduwayo mkuu wa tarafa ya Buyengero alitumwa gerezani siku ya jumatano majira ya saa kumi na moja akiambatana na baba yake mkwe ambaye ni mshahuri wa gavana anayehusika na fedha na utawala.

Wanatuhumiwa kosa la ubadilifu na wizi wa mabati na mifuko ya simenti iliyotolewa na ofisi ya rais wa jamuhuri ya Burundi kwa ujenzi wa shule.

Kwa mjibu wa vyanzo, viongozi wengine wengi wangetakiwa kuhojiwa katika kesi hiyo.

Previous Rwanda: spika wa baraza la seneti ajihuzuru
Next Bujumbura: gasoline shortage