Rwanda: spika wa baraza la seneti ajihuzuru

Rwanda: spika wa baraza la seneti ajihuzuru

Spika wa baraza la seneti alijihuzuru siku ya alhamisi jioni kwa sababu za kiafya. Dk Itamuremye Augustin alirejelewa kwa muda na naibu wake, na hivyo mabaraza mawili ya bunge na seneti kuongozwa na watu wa jinsia ya kike. Mwezi septemba uliopita alifanya ziara nchini Burundi. HABARI SOS Médias Burundi

Kwanza, ni bunge la Rwanda lililotoa taarifa za kuacha kazi kwa spika huyo wa baraza la seneti.

” mapema katika siku ya ijumaa, spika wa baraza la seneti Daktari Augustin Iyamuremye aliwasilisha barua ya kujihuzuru kama spika wa baraza la seneti kwa sababu za kiafya”, lilifahamisha tangazo la seneti la Rwanda siku ya alhamisi jioni.

Baraza la seneti lilizidi : ” ijumaa tarehe 9 disemba, katika kikao maluum kilichoitishwa kutangaza nafasi wazi ya spika wa baraza la seneti”.

Katika barua yake ya kujiuzuru iliyotumwa kwa naibu wa spika wa baraza la seneti, Iyamuremye alimushukuru rais wa Rwanda Paul Kagame kwa uaminifu wake kwake na kwa wajumbe wa baraza la seneti kwa kumuunga mkono wakati wa muhula wake.

” Ninajihuzuru kwenye uwadhifa wa spika wa baraza la seneti….kwa sababu za kiafya kwa vile ninatakiwa kuchukuwa muda wa kujitibisha bila kuharibu shughuli za baraza hilo. Ninachukuwa nafasi hii ili kuomba msamaha mahala ambapo sikuweza kutekeleza majukumu yangu vizuri. Hata hivyo nitaendelea kuleta mchango yangu hata kama nitakuwa nje ya ofisi ” , alifamisha mjumbe huyo wa zamani wa baraza la seneti.

Waziri huyo wa zamani wa itifaki na mfuasi mwenye ushawishi wa chama cha kijamii na demokrasia( PSD), Iyamuremye alichuwa nafasi hiyo ya spika wa baraza la seneti mwezi oktoba 2019.

Zaiara nchini Burundi

Mwezi septemba uliopita, Daktari Iyamuremye Augustin alifanya ziara nchini Burundi kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili za maziwa makuu.

Ni mwenzake wa Burundi Emmanuel Sinzohagera aliyempokea ofisini mwake.

” Tumepokea kwa mazungumzo ujumbe kutoka Rwanda unaoongozwa na Iyamuremye Augustin spika wa baraza la seneti. Mazungumzo yetu yameangazia uhusiano kati ya nchi hizi mbili na ametualika kushiriki katika kikao cha bunge la UIP mwezi octoba ujao”, alihakikisha bwana Sinzohagera.

Na ujumbe wa wa wabunge kutoka Burundi uliitikia mwaliko huo na kupokelewa pia ofisini mwake na spika wa baraza la seneti aliyeacha kazi.

” Tuna matumaini kuwa uhusiano mzuri utarudi hivi karibuni na ni wananchi wetu ambao watanufaika. Ishara muhimu itaonekana badaye kama tulivyoyaongelea na ma seneta kutoka Burundi ” , alisema hayo wakati huo Daktari Iyamuremye.

Katika miezi miwili iliyofuata, mipaka kati ya hizo nchi mbili ilifunguliwa rasmi.

akiongoza baraza la seneti, kiongozi huyo wa miaka 76 ni kiongozi wa pili baada ya rais wa jamuhuri. Iyamuremye aliacha nafasi hiyo baada ya kuongoza mkutano wa jumatatu wa kuhitimisha vikao vya baraza la seneti vya wiki hii.
Wajumbe wa baraza la seneti hilo la watu 26, wako na hadi siku 30 ili kumuchagua mkuu mpya wa baraza hilo.

Kwa kusubiri, Espérance Nyirasafari, naibu wa spika wa baraza la seneti anayehusika pia na sheria na kufuatia shughuli za serikali ndie anaongoza baraza hilo kwa muda.

Ikimbukwe kuwa baraza la bunge pia kinaongozwa na mwanamke.

Rais Paul Kagame angetakiwa kumuteuwa seneta mwingine kwa ajili ya kuchukuwa nafasi ya Iyamuremye hadi mwisho wa muhula wake mwaka wa 2024.

Iyamuremye amekuwa kwenye uringo wa kisiasa kwa miungo minne. Tangu 1994, alikalia nafasi nyingi za uongozi ndani ya ofisi ya rais hasa afisa habari na mambo ya nje.
Alikuwa pia mjumbe wa baraza la seneti la kwanza kwa kipindi cha miaka nane na kuhudumu kama mshahuri wa rais na nyadhifa zingine.

Kabla ya kuwa mjumbe wa baraza la seneti katika mwaka wa 2019, Iyamuremye alikuwa mkuu wa jukwa la ushahuri wa watu wa zamani wa Rwanda

Previous Busoni: discovery of a body
Next Rumonge: mkuu wa tarafa ya Rumonge amukuta mwenzake wa tarafa ya Buyengero gerezani