Mkutano wa Nairobi: serikali ya Kongo inasema ni fursa ya mwisho kwa makundi ya silaha

Mkutano wa Nairobi: serikali ya Kongo inasema ni fursa ya mwisho kwa makundi ya silaha

Mjumbe maluum wa serikali ya Kongo katika mazungumzo ya Nairobi anatahadharisha makundi ya waasi ambayo hataheshimu makubaliano ya Nairobi. Watajikuta wakitokomezwa na kikosi cha kikanda alitahadharisha Serge jumatano hii. Mpatanishi katika mzozo wa Kongo upande wake anaona kuwa ni wakati mwafaka kwa raia wa Kongo wenyewe kunufaika na utajiri wao. HABARI SOS Médias Burundi

Serge Tshibangu hakuzungumza kwa mafumbo: kila kundi la waasi ambalo halishiriki katika mazungumzo haya au ambalo halitaweka silaha chini baada ya mazungumzo ya Nairobi wanajikokotea hasira ya kikosi cha kikanda. Anayaomba kuzingatia kwa makini vitisho hivyo.

“[….], Wale ambao ni makundi ya silaha na yanayoshirikiana na makundi mengine ambayo hayako hapa, fikisheni ujumbe : wakati huu mwafaka ambapo wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki bado wanawapokea na bara linalotuangalia, natumai ni wakati mzuri wa kujiunga na mchakato huu. Hatutaki kuwaona wa ndugu zetu waliochukuwa silaha kwa sababu yoyote wakitokomezwa na kikosi cha kikanda kwa sababu tu ya kuacha kuchukuwa fursa walipewa, alifahamisha.

Kwa mjibu wa Bwana Tshibangu, kutohudhuria kwa M23 katika mazungumzo hayo ya Nairobi haiwezi kuwa kizuizi katika kupata suluhu ya mzozo wa mashariki mwa Kongo.

” Nataka kuwahakikishia jambo moja, hali inayoshuhudiwa kwa sasa na kundi la M23 haitasimamisha mchakato wa Nairobi. Mchakato wa Nairobi hawukuanzishwa kwa ajili ya M23″, alifafanua mjumbe maluum wa Kinshasa.

Mpatanishi katika mzozo wa Kongo upande wake, anasema kuwa ni wakati mwafaka kwa raia wa DRC kunufaika na utajiri wao. Uhuru Kenyatta pamoja na kukumbusha kuwa ni jukumu la raia wa Kongo wenyewe kutafuta suluhu ya matatizo yao, analaani kuwa ni mzozo unaendelea na kuliweka taifa katika umasikini.

” Tunafahamu kuwa wa ndugu zetu wa Kongo wanakabiliwa na mzozo usiomalizika kwa zaidi ya miaka 20. Kuna watoto ambao hawajaona mlango wa shule kutokana na vita, wanaume ambao hawajawahi kupata fursa ya kuendesha kilimo na kupata chakula na hivyo kujiondoa katika umasikini sababu ya vita. Kuna utajiri mwingi ambao Mungu aliwakabidhi chini ya ardhi yenu lakini unazalishwa na wageni kutokana na vita. Ni wao wanaonufaika na utajiri huo wakati ambapo watoto wenu hawawezi hata kwenda shule, akinamama hawana hospitali au malaha pazuri pa kuzaa watoto. Na watu wanaishi kama wakimbizi katika nchi yao”, analalamika.

Wakati viongozi wa Kongo wakiendelea kutuhumu Rwanda kuunga mkono M23, rais mstaafu wa Kenya anatoa ushahuri wa mataifa hayo mawili ya kanda ya maziwa makuu kuzidi kukumbuka kuwa ni majirani wanaolazimika kuishi pamoja.

” Tunaweza kuwachagua marafiki lakini Mungu hakutupatia uhuru wa kumchagua jirani “, alisisitiza.

Jumatano hii, rais wa Rwanda Paul Kagame amerejelea uhusiano mbaya kati ya nchi yake na nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati.

[….]…sasa hawa watu wanaofikiria sisi ni migomba mifupi…lakini bwana wanajidanganya….” amesema hayo akizungumza kwa kiswahili na kingereza kwa sauti kali . Ilikuwa kando na sherehe za kuapishwa kwa waziri mpya wa afya.

Na kusisitiza akipigiwa makofi na wajumbe wa baraza la bunge kuwa :” sisi kwa kwa ufupi wetu hatuna uwezo lakini tuna njia…na tuko imara hujajuwa, hujuwi, unaweza ukaelewa imara tulivyo “.

Previous North Kivu: a dozen fighters captured
Next Nyanza-Lac: the communal administrator and all his aids sacked