Kivu-kusini: majeshi ya Burundi na Kongo yafahamisha kukimbiza waasi wa FNL

Kivu-kusini: majeshi ya Burundi na Kongo yafahamisha kukimbiza waasi wa FNL

Mapigano yariporitiwa eneo la Mwenga tangu alhamisi 24 novemba. Ni katika kitongoji cha Itongwe mkoa wa kivu ya kusini. Majeshi ya Burundi na Kongo yanafamisha kuwa yaliwauwa angalau waasi 40 na kuchukuwa udhibiti wa ngome za kimkakati za FNL (waasi wa Burundi) chini ya uongozi wa jemedali Aloys Nzabampema. Kiongozi huyo wa waasi hao hakupatikana ili ajieleze kuhusu taarifa hizo. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na vyanzo vya ndani katika vijiji vya Mugunda na Maheta, mapigano yaliripotiwa katika misitu ya Namaramara na Naombi. Ni eneo hilo ambako kuna makao makuu ya kijeshi ya waasi wa FNL ya Aloys Nzabampema.

Kupitia tangazo, jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) lilifahamisha kuwa muungano wa jeshi hilo na jeshi la Burundi ulishambulia ” adui” na kumufukuza katika milima yote nne juu ya kitongoji cha Naombi ambacho awali kilikuwa ngome kuu na kituo cha kukusanyia misaada na mahitaji ya waasi wa Nzabampema.

” Adui baada ya kufukuzwa, amekimbia na anajificha katika msitu wa Itongwe eneo la Mwenga baada ya kupoteza idadi kubwa ya wapiganaji na vifaa ( waasi 40 wameuwawa) yamesomeka ndani ya tangazo lililosainiwa na luteni Marc Elongo msemaji wa kikosi cha opereshini Sokola 2.

Luteni Elongo anasema ni operesheni ya kwa “undani” ili kutokomeza kabisa kundi na kuliweka katika hali ya udhaifu”

Majeshi ya Burundi na Kongo yanashirikiana rasmi tangu septemba iliyopita ” kukabiliana na makundi ya silaha ya ndani na nje ya nchi ” katika mkoa wa Kivu ya kusini. Ni chini ya kikosi cha kikanda kilichanzishwa na wakuu ya nchi za jumuiya ya afrika mashariki mwishoni mwa juni mwaka huu. Katika eneo hilo la Kongo, kunaripotiwa makundi mawili ya waasi kutoka Burundi ambayo ni FNL na Red Tabara yanayochukuliwa na viongozi wa Burundi kama makundi ya kigaidi.

Hivi karibuni, rais wa Burundi alifahamisha kuwa makundi mengi ya silaha katika mkoa wa Kivu ya kusini yalikubali kuweka silaha chini. Kwa tikiti cha mwenyekiti wa EAC, alikuwa akimpokea mpatanishi katika mzozo wa Kongo rais wa mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Jemedali Nzabampema na msemaji wake hawakupatikana ili kujieleza juu ya habari hizo. Lakini mwishoni mwa mwezi septemba, alihakikishia SOS Médias Burundi kuwa ” wanajeshi wa Burundi na Kongo walishambulia ngome za wanajeshi wetu”. Alikiri kuwa walirudisha nyuma ” uvamizi huo” na kuwauwa askali jeshi na wengine kukamatwa”. Makabiliano hayo yalisababisha angalau wananchi elfu tatu kukimbia kwa mjibu wa vyanzo vya ndani.

Mapigano kati jeshi la FARDC-FDNB ( jeshi la Burundi) na waasi wa FNL wa jemedali Aloys Nzabampema yameibuka wakati ambapo jumatatu hii mazungumzo kati ya serikali ya Kongo na makundi mbali mbali ya waasi yakianza mjini Nairobi makao makuu ya Kenya. M23 kundi la waasi linalodhibiti maeneo mengi katika mkoa wa Kivu kaskazini likiwemo jiji la Bunagana, linalopakana na Uganda tangu 13 juni na ambalo limekubali kuweka silaha chini tangu ijumaa tarehe 25 novemba halihusishwi na mchakato huo.

Bertrand Bisimwa kiongozi wa kundi hilo alifahamisha kupitia tangazo kuwa ” M23 linaomba kukutana na mpatanishi ili kuongelea mambo yanayomuhusu […] na hivyo amani ya kudumu yaweze kurejea katika nchi yetu”.

Ilikuwa baada ya kikao cha Luanda (Angola) kilichofanyika wiki hii na kujadili mzozo wa mashariki wa Kongo, hasa swala la kundi la M23.

Previous Tanzania: more than 12,000 people without latrines in Nduta and Nyarugusu camps
Next Photo of the week-Burundi: the ICC wants to take the next step