DRC: M23 inatuhumu serikali kuvunja makubaliano ya kusitisha vita na kuwauwa raia wa kawaida

DRC: M23 inatuhumu serikali kuvunja makubaliano ya kusitisha vita na kuwauwa raia wa kawaida

Kulingana na tangazo la jumatano hii, kundi hilo la waasi linatuhumu jeshi la Kongo kujiunga na makundi ya silaha likiwemo kundi la Mai Mai na FDLR ili kuwauwa raia wa kawaida. Kundi hilo linatahadharisha juu ya kuwepo kwa mauwaji ya kuangamiza na kuhakikisha kuwa “Hatutalea mikono wakati raia wakiendelea kuuwawa”. HABARI SOS Médias Burundi

Kundi la M23 linasema kuwa kuna mauwaji ya kuangamiza yanayoendelea na mauwaji mengine yanayotekelezwa na muungano wa serikali.

Kundi hilo linaloshukiwa kuwauwa angalau raia wa kawaida 272 wiki iliyopita, linakiri kuwa jeshi la Kongo na washirika wake walivamia ngome zake eneo la Bwiza na maeneo ya karibu kwa kukiuka usitishwaji wa vita unaoendelea ” .

” Muungano huo ulijihusisha na kuwauwa wananchi wasiokuwa na hatia kwa kuteketeza nyumba zao, kupora na kuchinja mifugo yao kwa uharibifu” linasema Kundi la waasi ambalo pia linazidi kuwa” mashambulizi hayo yalisababisha majeruhi mengi na wakimbizi wa ndani”.

Kundi hilo waasi wa kabila la watutsi ambalo lilichukuwa silaha tena mwishoni mwa 2021 linatuhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi zao kuhusu kuwarudisha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake.

” inatakiwa kujulikana kuwa kuna mauwaji ya kivizia Kabila wa watutsi na wale wasiounga mkoani itikadi hiyo ya ubaguzi […] wakati jamii ya kimataifa ikisalia kimya. Inaturudisha katika enzi za mauwaji ya 1994 ya kuangaliza jamii ya watutsi nchini Rwanda yaliotekelezwa na moja kati ya washirika wa serikali ya Kinshasa….”.

M23 katika tangazo lake linaomba baraza la usalama la umoja wa mataifa, umoja wa ulaya na afrika, EAC na wengine kuingilia kati.

Linawaomba kuchukuwa maamuzi mara moja dhidi ya mauwaji hayo yanayoendelea na kwa ” mashirika ya kimataifa kuingilia kati na kutoa misaada wa familia za wakimbizi wa ndani ambao idadi yao inazidi elfu sita waliopata hifadhi katika maeneo chini ya udhibiti wa kundi letu”.

Tangazo hilo la M23 lililosainiwa na Lawrence Kanyuka msemaji wa kisiasa wa kundi linazidi kusema kuwa M23 haitasalia mikono ikiwa imeshikana wakati raia wakiendelea kuuwawa”, na kusisitiza kuwa ” wako tayari kuingilia kati ili kusimamisha mauwaji hayo ya kutisha “.

Tangazo hilo lilitolewa wakati ambapo waziri wa sheria wa Kongo alipokelewa na mwendeshamashtaka wa mahakama ya ICC( mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita) mjini the Hague ili kuzungumzia kisa cha mauwaji ya Kishishe yaliodaiwa kutekelezwa na M23 na Rwanda. Serikali ya Kongo ilifahamisha jumatatu hii kuwa angalau watu 272 waliuwawa wakiwemo watoto 17 wakati wa janga hilo.

Previous Ruyigi: Rwandan nationals targeted by arrests
Next DRC: mkasa wa mauwaji ya kishishe kupelekwa mbele ya ICC