DRC: mkasa wa mauwaji ya kishishe kupelekwa mbele ya ICC

DRC: mkasa wa mauwaji ya kishishe kupelekwa mbele ya ICC

Waziri wa sheria ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo jumatano hii alipokelewa na mwendeshamashtaka wa ICC ili kuzungumzia swala la mauwaji ya Kishishe (mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki wa DRC). Anaomba ICC kuanzisha uchunguzi juu ya mauwaji hao yanayodaiwa kutekelezwa na waasi wa M23. Kinshasa inazidi pia kuwa ni “kosa la uvamizi ambalo lilitekelezwa na Rwanda”. HABARI SOS Médias Burundi

Maovu hayo yalitokea eneo la Kishishe, Kijiji cha Kivu kaskazini, kwenye umbali wa kilometa 70 tarehe 29 novemba iliyopita. Jeshi la Kongo lilituhumu mara moja waasi wa M23 kutekeleza mauwaji hao ya ” angalau watu 50″ , idadi ambayo iliongezwa na Kongo siku ya jumatatu. Ilifahamisha kuwa idadi ya waliuwawa inafikia watu 272 wakiwemo watoto 17.

Kinshasa inahakikisha kuwa jeshi lake halikuwa maeneo hayo wakati wa tukio hilo.

Kundi hilo la waasi lilikanusha madai hayo ya viongozi wa Kongo na kukubali kuwa wananchi nane walikufa katika kijiji hicho kwa kupituliwa na risasi zilizopoteza shabaha wakati wa mapigano na waasi wa Mai Mai na FDLR.

Mkasa huo mbele ya ICC

Jumatano, waziri wa sheria wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo alipokelewa na mwendeshamashtaka wa korti ya kimataifa ili kuzungumzia swala la Kishishe.

” Wakati tukiwa hapa, sehemu ya ardhi ya mashariki mwa DRC imekuwa uwanja wa uhalifu dhidi ya binadamu na wa kivita” , alifahamisha Rose Mutombo Kiesse akitumia fursa ya kikao cha 21 cha serikali zilizosaini mkataba wa Roma na kuomba ICC ” kuchukuwa jukumu lake nchini DRC na kuanzisha uchunguzi juu ya mauwaji hayo.

Kinshasa ina mpango wa kuishtaki Rwanda mbele ya sheria hiyo ya kimataifa.

” Lilifanyika pia kosa la uvamizi lililopelekea ma mia ya watu kufariki dunia, unyanyasaji wa kijinsia bila kuhesabu idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani. Wanaofanya vitendo hivyo wanajulikana : ni kundi la ADF na M23 ambao ni washirika wa jeshi la Rwanda. Nchi hiyo inatakiwa kuwajibishwa na kulipa mbele ya korti ya ICC”, alizidi kusema

Baada ya mkutano wa waziri wa Kongo wa sheria mjini the Hague, ICC haikutaka kutangaza chochote na kudai kuwa bado ni mapema”.

Hata hivyo, mwendeshamashtaka wa korti hiyo Karim Khan, alifahamisha kuwa ” hivi karibuni ana mpango kutembelea baadhi ya nchi ” bila kutaja nchi hizo.

Lakini kwa mjibu wa viongozi wa Kongo, ” mwendeshamashtaka kutembelea nchi ya Kongo itamuwezesha kushuhudia janga la kibinadamu linaloripotiwa na hivyo kuacha kusita kufungulia mashtaka wahusika na washirika wao waliofanya uhalifu huo mkubwa”.

Upande wake, Kigali inatupilia mbali madai ya kuunga mkono M23 na kutuhumu jamii ya kimataifa kuchochea mzozo wa mashariki mwa DRC.

Wakati wa mazungumzo yake na rais wa Rwanda Paul Kagame kupitia simu siku jumapili, katibu mkuu wa serikali ya Marekani Antony Blinken alisema moja kwa moja kuwa ” misaada yote kwa makundi ya silaha ya nje nchini DRC inatakiwa kusimama ukiwemo msada wa Rwanda kwa M23″, kulingana na msemaji wa serikali ya marekani Ned Price, kwa mjibu wa tangazo.

Badaye, waziri wa Rwanda wa mambo ya nje Vincent Biruta alithibitisha kuwa rais Paul Kagama na Anthony Blinken walikuwa na mazungumzo mazuri (….) lakini tofauti zilionekana wakati wa kuelewa tatizo”.

” Njia isio kuwa ya uhakika iliyochikuliwa na jamii ya kimataifa inasababisha tatizo hilo kuwa gumu ” aliendelea waziri wa diplomasia wa Rwanda.
Vincent Biruta alifahamisha kuwa ” matatizo ya usalama wa Rwanda yanatakiwa kuzingatiwa” na kuendelea kuwa M23 haiwezi kufananishwa na Rwanda”.

” Jukumu linatakiwa kuwekwa mahala pale ili kutafuta suluhu la kudumu” alizidi kusema bwana Biruta.

Kwanza, alisema, ” ni kutowajibika kwa serikali ya DRC na taasisi zake na uungwaji mkono wake kwa kundi la FDLR. Harafu watu wa nje kujihusisha na mzozo huo na juhudi za kimataifa na za bara zinasaidia kulinda DRC na kulishawishi taifa hilo kutoheshimu ahadi zake katika mchakato unaoendelea “.

” M23 haiwezi kufananishwa na Rwanda. Sio tatizo linalotakiwa kusuluhishwa na Rwanda” alikumbusha.

Na kusisitiza kuwa :” wasi wasi wa Rwanda kuhusu usalama wake unatakiwa kuzingatiwa, na iwapo wengine hawaoni kama ni jukumu lake, Rwanda itaendelea kuwajibika”.

Wakati huo, mazungumzo ya Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kujaribu kusuluhisha mzozo wa Kongo yalimalizika jumanne, M23 ikiwa halikualikwa hali ambayo ilikosolewa na wataalam wa maswala ya siasa.

M23 ni kundi la zamani la waasi wa kabila la watutsi lililochukuwa silaha tena mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi zake kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake. Tangu juni iliyopita, lilichukuwa maeneo mengi ya Kivu-kaskazini likiwemo eneo la Bunagana, mji wa mpakani na Uganda. Hivi karibuni kundi hilo lilifahamisha kuwa limesitisha vita kufuatia matokeo ya mkutano wa Luanda (Angola). Lakini linatuhumu jeshi la Kongo na washirika wake kukiuka makubaliano na kuwauwa raia wa kawaida.

Previous DRC: M23 inatuhumu serikali kuvunja makubaliano ya kusitisha vita na kuwauwa raia wa kawaida
Next Rumonge: the district administrator joins his colleague from Buyengero in prison