Ituri/Kivu-kaskazini: miili ya raia wa kawaida 27 waliouwawa na wapiganaji wa ADF imepatikana katika eneo la Irumi na Béni
Miili 2O ya watu waliouwawa na waasi kutoka Uganda wa ADF (kundi la waasi) iligunduliwa katika vijiji vingi vya eneo la Irumi mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC. Maiti zingine saba zilipatikana katika wilaya ya Beni ndani ya mkoa jirani wa Kivu-kaskazini. Waasi kutoka Uganda wanaendelea kusababisha hofu na majonzi katika upande huo wa Kongo licha ya ongezeko la operesheni za pamoja kati ya jeshi la Kongo na Uganda. Miili hiyo iligunduliwa mwanzoni mwa wiki hii. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa mratibu wa shirika la makubaliano kwa ajili ya kuheshimu haki za binadamu (CRDH), tawi la Irumi Christophe Munyanderu, ni vijiji vya Epanza, Kazaroho, Ntume na Mangwalu vilivyoorodhesha idadi kubwa ya maafa.
” Watu wengi waliuwawa na waasi wa ADF wiki iliyopita ndani ya msitu unapatikana magharibi mwa kijiji cha Otomabere ni katika wilaya ya Bandavilemba kanda ya Walese-Vonkutu. Ni vigumu vya familia zilizoathiriwa kupata maiti za wajumbe wao. Jumapili iliyopita, baadhi ya watu wa kujitolea walijaribu kwenda kuchukuwa miili ya raia waliouwawa eneo la Kazaroho. Baada ya kufika kwenye kituo cha Epanza, walikuta ADF wakiandaa chakula karibu na kijiji hicho. Walituhakikishia uwepo wa watu wa ADF karibu na kijiji” alibaini Christophe Munyanderu.
Watu wengine saba waliuwawa na waasi hao katika vijiji vya Kamungu, Maisafi, kambi ya chui, Kanana, maeneo ya karibu na tarafa ya Eringeti wilayani Beni katika mkoa wa Kivu-kaskazini jirani na mkoa wa Ituri. Waliuwawa katika mashambulizi ya jumamosi na jumapili kulingana na wafanyakazi wa serikali eneo la Eringeti.
” Tulizika miili ya watu saba jumatatu katika eneo la tukio. Wahanga waliuwawa na waasi wa ADF baadhi katika siku ya jumamosi na wengine jumapili iliyopita. Hadi sasa watu wengine haijulikani walipelekwa wapi. Ni matokeo ya muda, alithibitisha Sabiti Njiamoja , mfanyakazi wa serikali.
Mashirika ya kiraia ya eneo hilo yanathibitisha habari hizo na kuzidi kuwa raia wengine walitekwa na waasi.
Yanahakikisha kuwa waasi walichoma moto mali za raia na nyumba katika vijiji vilivyoshambuliwa.
” Hali ni mbaya zaidi katika vijiji vya Maisafi, Kambi ya chui, Kanana. Mbali na raia kuuwawa, angalau wengine 30 haijulikani mahala waliopo. Waasi walichoma moto mali za wananchi kabla ya kuondoka dakika chache badaye, harafu wakarudi tena” , alifahamisha Bravo Vukulu, mmoja kati ya washahuri wa shirika la kiraia la Bambuba-Kisiki.
Kutokana na hali hiyo, mjumbe wa serikali eneo la Eringeti anawatolea mwito raia wa eneo hilo kuonyesha kila mtu anayeleta wasiwasi. Waakazi wa eneo hilo wanahofia kutokea mashambulizi mengine.
” Tumeokota vijikaratasi barabarani vinavyoarifu kuhusu uwezekano wa kuwepo mashambulizi katika siku ya chrismasi na mwaka mpya.
About author
You might also like
North Kivu : 48 hours is the ultimatum set by local armed groups to the regional force to leave the DRC
This Wednesday, local armed self-defense groups issued an ultimatum to the regional EAC force to leave its positions in Masisi, Rutshuru and Nyiragongo. It is in the province of North
Nyanza-Lac : three men arrested and taken to an unknown destination
Three men were arrested on Saturday, May 18, by the head of the National Intelligence Service (SNR) in Nyanza-Lac and the provincial police commissioner, after a search of their home.
North Kivu: lull calm in Sake after a day under high tension
The fighting between the D.R Congo army and the M23 rebels in the city of Sake, in the territory of Masisi in the province of North Kivu (in the east