Kirundo: nani kamuuwa Kambayingwe mkimbizi huyo aliyerudi nchini ?

Kirundo: nani kamuuwa Kambayingwe mkimbizi huyo aliyerudi nchini ?

Watu wanne akiwemo katibu wa chama cha CNDD-FDD mkoa wa Kirundo (kaskazini mwa Burundi) na muakilishi wa tawi la vijana wafuasi wa chama tawala ngazi ya mkoa wanatajwa kuhusika katika mauwaji ya Ferdinand Nyandwi maarufu Kambayingwe mkimbizi wa zamani mkaazi wa kambi ya Mahama nchini Rwanda. Mke wa marehemu aliyeshuhidia tukio la kutekwa kwa mumeo alitoa ushuhuda wake tarehe 6 disemba katika mkutano ulioongozwa na waziri mkuu Gervais Ndirakobuca. Alitaja waliohusika katika kifo cha mume wake. HABARI SOS Médias Burundi

Mjane huyo alibaini baadhi ya majina ya watu ambao aliwaona.

” Niliona polisi mlinzi wa katibu wa chama cha CNDD-FDD ngazi ya mkoa Jean Claude Mbarushimana na mkuu wa Imbonerakure Abel Ahishakiye. Askali polisi wakiwa pamoja na viongozi wao walimpiga sana mume wangu […] alifafanua mjane huyo.

” Walikanyaga sehemu zake za siri, mbavu zake na kichwa,…” , alibaini mama huyo wa watoto watano.

Vyanzo vinasema kuwa ingawa muathiriwa alituhumiwa kumiliki silaha kinyume cha sheria, ulikuwa ni uongo.

” Walitafuta tu sababu za kumumalizia maisha”, vinahakikisha vyanzo vyetu.

Wawakilishi wa chama cha CNDD-FDD mkoani Kirundo wanamutuhumu Kambayingwe ” kushiriki katika mandamano ya 2015 dhidi ya muhula wa kutatanisha wa tatu wa hayati Pierre Nkurunziza”.

Mfuasi huyo wa zamani wa chama cha UPD Zigamibanga ( upinzani) huenda akawa alimpiga kamishena ya polisi wa kipindi hicho wakati akijaribu kumkamata. Wakati ambapo alipoanza kutafutwa, Kambayingwe alikimbilia nchini Rwanda.

Aliporudi kutoka kambi ya Mahama mwaka uliopita, Kambayingwe, aliwasogelea wafuasi wa chama tawala ili kuweza kutekeleza kwa amani mradi wake wa kutengeneza biya kutoka matunda mbali mbali.

Vyanzo vingine vinamuhusisha pia mkuu wa tarafa ya vumbi Viateur Habimana katika mauwaji hayo.

” Ni yeye aliyetoa gari ya kubeba watu watatu akiwemo mjane kushiriki katika mazishi yaliyolazimishwa na viongozi mkoani Kirundo. Muili wa muhanga ulikuwa umetupwa katika msitu wa Murehe karibu na mpaka kati ya Burundi na Rwanda. Alifanya hivyo ili kujionyesha lakini yuko miongoni mwa waliotoa amri ya mauwaji hayo, walisema.

Mke wake anaomba haki itendeke licha ya kukabiliwa na vitisho na kunyamanzishwa.

” Magari ya katibu wa mkoa wa chama na ile ya mkuu wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD huwa inafanya nenda rudi mbele ya nyumba yangu. Wakiwa pamoja na askali polisi wanakuja kunitisha, alimufahamisha waziri mkuu Gervais Ndirakobuca.

Waziri mkuu alitoa amri kwa gavana wa mkoa kulinda usalama wa mjane huyo.

Licha ya kutangazwa kwa majina ya waliohusika na mauwaji hayo, hakuna uchunguzi ulioanzishwa, analaani mtu wa karibu na faili hiyo.

Kisa cha Kambayingwe ni moja kati visa vya mauwaji ya wakimbizi waliorejea nchini ambavyo wakimbizi katika kambi ya Mahama nchini Rwanda waliibua jumanne hii wakati ujumbe wa serikali ya Burundi ukikutana na wakimbizi hao wanaosita kurudi katika nchi yao.

Ferdinand Nyandwi maarufu Kambayingwe aliuwawa tarehe 26 novemba na maiti yake kutupwa ndani ya msitu wa Murehe si mbali sana na mpaka na Rwanda. Alizikwa ghafla kwa amri ya viongozi tawala na polisi mkoani humo.

Previous Ituri/Kivu-kaskazini: miili ya raia wa kawaida 27 waliouwawa na wapiganaji wa ADF imepatikana katika eneo la Irumi na Béni
Next Bujumbura: the fuel crisis far from being resolved