Muyinga: moshi unaotokana na viripuzi vinavyotumiwa katika migodi ya dhahabu husababisha maradhi ya mapaafu na kifo

Muyinga: moshi unaotokana na viripuzi vinavyotumiwa katika migodi ya dhahabu husababisha maradhi ya mapaafu na kifo

Wakaazi wa kijiji cha Kamaramagambo tarafani Butihinda mkoa wa Muyinga (kaskazini mashariki mwa Burundi) wanasema kuwa moshi unaoletwa na viripuzi vinavyotumiwa kuvunja mawe makubwa ndani ya migodi na kusababisha maradhi ya mapaafu ni tishio kubwa kwao. Mungurumo wa viripuzi hivyo huwaathiti akinamama wajawazito na watu wenye matatizo ya moyo pia. Wakaazi wa kijiji cha Kamaramagambo wanaoomba zitumiwe mbinu ambazo hazileti athari “kwa afya yetu” au shughuli hiyo isimamishwe. HABARI SOS Médias Burundi

Chanzo chetu tarafani Butihinda katika kijiji cha Kamaramagambo kinahakikisha kuwa raia wakaazi wa kijiji hicho na maeneo ya karibu wanakabiliwa na tishio la moshi unaosababishwa na viripuzi vinavyotumiwa kuvunja mawe makubwa ya migodini.

Watu wanaokadiriwa kuwa na kumi ya watu walifariki dunia tangu mwaka wa 2015 kutokana na maradhi ya mapaafu yaliyosababishwa na moshi wa viripuzi hivyo.

” Ni raia wenye asili ya Tanzania walioanzisha mbinu hiyo, nadhani ilikuwa mwaka wa 2013. Iwapo mripuko umetokea, wachimba migodi wanaharakia kuingia kwa ajili kuchukuwa vipande vya mawe vilivyochanganywa na dhahabu. Tulikuwa hatujuwi kuwa maisha yao yako hatarini ” analalamika mwanamke wa miaka takriban 30.

” Tumekuwa wajane kutokana na viripuzi hivyo na watato wetu wamekuwa mayatima. Waume zetu walijitibisha katika hospitali ghali hapa nchini na hata nje ya nchi hususan nchini Rwanda, India lakini mwisho walikufa kutokana na maradhi hayo ya mapaafu”, analaani mjane mmoja ambaye kwa sasa anaishi kwenye makao makuu ya Muyinga.

Vyanzo vyetu eneo la Kamaramagambo vinaarifu kuwa kutokana na viripuzi hivyo, akinamama wajawazito wanakabiliwa na hatari ya kuzaa kabla ya wakati.

” Tunakabiliwa na hatari ya kila siku ya mimba kuporomoka wakati wa ujauzito kutokana na mungurumo ya viripuzi hivyo “, amabaini mwanamke mwingine.

Watu wengine ambao wako hatarini ni wale wenye matatizo ya moyo. Watoto wachanga pia wanahofiwa. Wakaazi wa Kamaramagambo wanaomba zitumike mbinu zingine ambazo sio hatari kwa maisha ya watu.

” Na kama hawawezi kufanya hivyo, basi mgodi huo ufungwe mara moja sababu maisha yetu yako hatarini”, walibaini.

“Hata hivyo wachimba dhahabu hawakubaliani na sisi.” Wanafahamisha kuwa wako na ruhsa ya wizara ya biashara inayotoa idhini kwa kuchimba migodi wanaojumuika katika vyama vya ushirika.

Msemaji wa wizara ya biashara na viongozi tawala hawakupatikana ili kujieleza juu ya kesi hiyo.

Previous Muyinga: smoke from explosives used in gold mines causes fatal lung poisoning
Next Nyarugusu (Tanzania): mpango wa chakula PAM (WFP) uligawa maharagwe yasioweka kutumiwa na wakimbizi